BIDHAA ZA KULINDA AFYA ZA GREEN WORLD

Kama tulivyokwishaona hapo nyuma kampuni ya Green world imewekeza katika uimarishaji wa afya ya binadamu kwa kiwango cha hali ya... thumbnail 1 summary








Kama tulivyokwishaona hapo nyuma kampuni ya Green world imewekeza katika uimarishaji wa afya ya binadamu kwa kiwango cha hali ya juu kabisa. Hili linathibitika kupitia mlolongo mkubwa wa bidhaa za namna tofauti tofauti zilizokwisha tengenezwa na zingine zinazozidi kutengenezwa na kampuni. Kwa sasa kuna zaidi ya aina 100 za bidhaa zilizokwisha tengenezwa na zinazotumiwa kwa maunfaa na watu wengi zaidi duniani.Kupitia uwepo wa bidhaa hizi maelfu ya watu Tanzania na mamilioni ya watu duniani wamenufaika sana kiafya.


Aina Za Bidhaa Za Green World

Bidhaa za Green world zimegawanyika katika makundi yafuatayo:

1.Bidhaa za akina mama
2.Bidhaa za wanaumme
3.Bidhaa za kuondoa sumu
4.Bidhaa za mwili
5.Mbolea ya maji

Kwa sababu ya kuongezeka kwa teknolojia kila siku kunapokucha na mabadiliko ya tabia ya nchi,afya ya mwanadamu imehatarishwa kwa kiwango kikubwa kabisa. Vyakula tunavyokula vingi vimekuwa vikiandaliwa katika mazingira na namna ambayo huhatarisha afya kwa ujumla. Wakati mwingine mfumo wenyewe wa kula tulio nao umeongeza hatari zaidi katika afya kuliko faida. Matumizi ya sumu katika kuandaa vyakula kama vile mbolea zenye sumu,mafuta mengi katika chakula,sukari nyingi katika chakula,chumvi iliyozidi na mengine mengi yamechangia kwa kiwango kikubwa kabisa kudhoofisha afya zetu. Kama hiyo haitoshi kuongezeka kwa uchafuzi wa mazingira kwa maana ya ardhi,maji na hewa bila kujali athari zake nako kumekuwa ni changamoto kubwa katika afya kwa ujumla wake. Kama hiyo haitoshi matumizi ya simu,komputa,TV,minara ya simu na microwave yamesababisha ongezeko la magonjwa na matatizo ya kiafya kwa ujumla kuwa kubwa.

Kwa kufahamu hilo kampuni ya Green world kupitia kwa muasisi wake, Dkt. Deming Li ikaamua kutengeneza bidhaa nyingi za kutosha baada ya utafiti wa muda mrefu. Bidhaa hizi husaidia kuondoa sumu mwilini (Detoxification),Kuondoa magonjwa ya mtindo wa maisha (Functional products) na bidhaa lishe (Food supplements products).






Baada ya utafiti wa muda mrefu bidhaa hizi sasa ni mkombozi kwa watumiaji walio wengi walikuwa na matatizo sugu na yanayotaabisha jamii sana. Leo matatizo kama shinikizo la juu la damu,magonjwa ya moyo,kisukari,kansa,magonjwa ya mishipa ya ubongo,vidonda vya tumbo,magonjwa ya mifupa,afya ya wanaume,afya ya wanawake,unene kupita kiasi na mengine mengi,yamekuwa tishio kwa wakazi wa Tanzania na dunia kwa ujumla.





Bidhaa za green world kwa bahati nzuri zina uwezo wa kukabiliana na changamoto hizi kwa kiwango cha juu kabisa na kumwacha mtumiaji akiwa na afya nzuri bila kusalia kwa kemikali yoyote baada ya matumizi. Utakubaliana nami kuwa bidhaa nyingi zitumiwazo kwa ajili ya ujenzi wa afya huongeza madhara zaidi kuliko faida. Lakini kwa uapnde wa bidhaa za green world,kwa jinsi unavyoendelea kutumia ndivyo unavyopata manufaa zaidi kuliko kutotumia.



Naamini kupitia maelezo haya ya kina kuhusu bidhaa za kampuni ya green world,utachagua kuimarisha afya yako kwa kutumia bidhaa hizi.