MAWE KWENYE FIGO-KIDNEY STONES

Mawe kwenye figo ni mrundikano wa vitu vigumu (madini na chumvi chumvi) kwenye figo. Mawe kwenye figo huweza kuathiri mfumo wa mkojo-k... thumbnail 1 summary




Mawe kwenye figo ni mrundikano wa vitu vigumu (madini na chumvi chumvi) kwenye figo. Mawe kwenye figo huweza kuathiri mfumo wa mkojo-kutoka kwenye figo hadi kwenye mfuko wa mkojo. Mara nyingi mawe kwenye figo hutengenezwa pale madini na chumvi chumvi zinapogandaman na kujisusanya ndani ya figo. Mawe haya kwenye figo huwa na ukubwa kama vimawe vya mchanga japo wakati mwingine huweza kukua na kufikia ukubwa wa mpira wa gofu kama hayajagunduliwa na kutibiwa mapema.

Kukojoa mkojo wenye mawe huweza kuwa na maumivu makali sana,wengine husema ni kama maumivu ya kujifungua. Na kama jiwe ni kubwa huweza kuziba njia ya mkojo n ahapa huhitajika upasuaji.

Hebu sasa tutazame kwa kina tatizo la mawe kwenye figo na jinsi unavyoweza kupata utatuzi na kinga dhidi yake:


Chanzo Cha Mawe Kwenye Figo



Tatizo la mawe kwenye figo halina chanzo kimoja bainishi japo kuna mambo mengi kadha wa kadha yanayoweza kuongeza hatari ya kupata tatizo hili. Mawe kwenye figo hutengenezwa pale mkojo wako unapokuwa na vitu vigumu vingi kama calcium,oxalate na uric asidi kuliko kiwango cha maji. Wakati huo huo mkojo wako unaweza kukosa vitu vinavyozuia vitu vigumu hivyo kuungana pamoja na kutengeneza mazingira ya mawe kwenye figo kutengenezwa.

Aina tofauti tofauti za vitu (madini na chumvi) visababishayo mawe kwenye figo,inatupelekea kuwa na aina za mawe kwenye figo. Hebu sasa tuangalie aina za mawe kwenye figo:

Calcium Stones. Tatizo kubwa la mawe kwenye figo huwa ni mawe ya calcium na mara nyingi huwa katika hali ya calcium oxalate. Oxalate kwa asili hupatikana kwenye vyakula kama vile matunda,mboga,karanga na chocolate kwa wingi lakini pia hutengenezwa kwenye ini.

Mfumo wa ulaji,dozi ya vitamini D kwa wingi,kufanyiwa upasuaji wa utumbo mwembamba na matatizo mbali mbali ya kurithi huweza kuongeza calcium au oxalate kwenye mkojo.

Calcium stones pia hutokea kwa mfumo wa calcium phosphate.


Struvite Stones. Mawe haya kwenye figo hutokea kama matokeo ya maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI). Mawe haya hukua haraka na huweza kuwa na dalili au viashiria kidogo sana

Uric Acid Stones. Mawe ya uric asidi hutengenezwa kwa watu wanaokunywa maji kidogo sana au wanaopoteza maji kwa wingi,wanaokula vyakula vyenye protein kwa wingi na wenye ugonjwa wa gout. Lakini pia matatizo kurithi huweza kusababisha mawe ya uric kwenye figo.

Cystine Stones. Mawe ya aina hii hutokea kwa watu wenye ugonjwa wa kurithi ambao husababisha figo kuondoa kiwango kikubwa cha aina fulani ya amino acid.


Sababu Hatarishi Za Mawe Kwenye Figo



Mambo yanayoweza kusababisha kupata mawe kwenye figo ni kama yafuatayo:


1. Historia ya mtu/ Familia. Kama kuna mwanafamilia amewahi kuwa na tatizo la mawe kwenye figo,unaweza kuwa katika hatari ya kupata hilo pia. Lakini pia kama umewahi kupata aina fulani ya mawe kwenye figo,uko katika hatari ya kupata aina nyingine ya tatizo.

2. Kukaukiwa maji mwilini (dehydration).Watu wanaoshindwa kunywa maji kwa wingi,huwa katika hatari ya kupata mawe kwenye figo. Lakini pia watu wanaopoteza maji kwa wingi,kupitia jasho na wanaoishi maeneo yenye joto kwa wingi,huwa katika hatari ya kupata mawe kwenye figo.

3. Aina fulani za Vyakula. Kula vyakula vyenye calcium na sodium kwa wingi,huongeza kiwango cha calsium kinachotakiwa kuchujwa na figo na hivyo kuongeza uwezekano wa kupata tatizo la mawe kwenye figo.

4. Unene au Uzito. BMI kubwa,ukubwa wa kiuno,uzito kupita kiasi vinahusishwa moja kwa moja na hatari ya kupata mawe kwenye figo.

5. Magonjwa ya mfumo wa chakula na Upasuaji. Upasuaji wa tumbo,vidonda vya mfumo wa chakula,kuhara sugu,huweza kusababisha mabadiliko kwenye mfumo wa chakula na kuathiri ufyonzwaji wa calsium na maji. Hii inaweza kuongeza hatari ya kupata tatizo la mawe kwenye figo.

6. Matatizo kama renal tubular acidosis,UTI na mengineyop huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo la mawe kwenye figo.


Dalili Za Mawe Kwenye Figo



Kwa mgonjwa mwenye mawe kwenye figo,si rahisi kugundua dalili mapema. Mara nyingi dalili za ugonjwa wa mawe kwenye mfuko wa nyongo,huonekana pale mawe yaliyo kwenye figo yatakapoanza kutolewa pamoja na mkojo. Na hapo utapata dalili zifuatazo:

-Maumivu kushoto na kulia, pande za chini ya mbavu na mgongoni

-Maumivu chini ya kitovu na kwenye nyonga

-Maumivu yanayokuja na kupotea

-Maumivu wakati wa kukojoa

-Mkojo wa pink,mwekundu au wa kahawia

-Kichefuchefu na kutapika

-Mkojo mchafu unaonuka

-Kujisikia hamu ya kukojoa kusikoisha

-Kukojoa mara kwa mara

-Kujisikia homa

-Kukojoa kidogo kidogo

Maumivu ya mtu mwenye tatizo la mawe kwenye figo huweza kubadilika badilika,kwa mfano,huweza kuhama kutoka eneo moja kwenda jingine,au huweza kuongezeka na kupungua kwa kadri mawe yanavyosafirishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


Jinsi Ya Kujikinga Na Tatizo La Mawe Kwenye Figo


Kujiweka katika hali njema ya kuepuka kupatwa na tatizo la mawe kwenye figo,fanya mambo yafuatayo:

Kunywa maji siku nzima. Kunywa maji kwa wingi kutakusaidia kukojoa mara kwa mara na kutoa mawe nje kwa njia ya mkojo. Kwa mfano watu wenye historia ya kifamilia kupata mawe kwenye figo,wanashauriwa kukojoa angalau lita 2.5 kwa siku. Kwa hiyo kwa kadri inavyowezekana kunywa maji mengi angalau glasi 8 au zaidi kwa siku.

Epuka kula vyakula vyenye oxalate kwa wingi. Kama umegundua una tatizo la mawe kwenye figo,basi unashauriwa kupunguza vyakula vyenye oxalate kwa wingi. Hivi ni kama spinachi,viazi vitamu,karanga,chai,pilipili nyeusi na vyakula vya soya.

Epuka chakula chenye chumvi na protini ya wanyama kwa wingi. Hii husaidia kupunguza mrundikano wa mawe kwenye figo zaidi.

Mada zitakazofuata tutatazama magonjwa mengine ya figo-ugonjwa gafla wa figo na ugonjwa sugu wa figo. Endelea kuwa nasi.

Jitahidi kumwona daktari kama una miongoni mwa dalili zilizoainishwa hapo juu. Kama umefanikiwa kupata tiba na unaendelea nayo pia ni vyema. Pia unaweza kuwasiliana nasi kupata virutubishi tiba vitakavyokusaidia kusafisha figo,kuikinga figo na madhara zaidi,kuondoa sumu kwenye figo na kukuepusha na madhara zaidi kwenye figo.


Kwa mahitaji ya kupata virutubishi vyetu vya afya ya figo tafadhali wasiliana nasi.


Kwa maoni,ushauri au maswali,tafadhali wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.