Maambukizi kwenye njia ya mkojo ndio ugonjwa tunaoita UTI. Ni maambukizi kwenye sehemu yoyote katika mfumo wa mkojo. Mfumo wa mkojo hujumuisha figo,mirija ya ureta,kibofu cha mkojo na mirija ya urethra. Mkojo hutengenezwa kwenye figo na kupitishwa kupitia mirija ya ureta kuingia kwenye kibofu cha mkojo,na kisha kutolewa nje ya mwili kupitia mirija ya urethra. Mara nyingi maambukizi hutokea sehemu ya chini ya mfumo wa mkojo- kwenye kibofu cha mkojo na mirija ya urethra.
Wanawake ndio huwa katika hatari kubwa ya kupata UTI kuliko wanaume kwa sababu ya maumbile yao. Maambukizi ya njia ya mkojo hasa kwenye kibofu huwa na maumivu makali japo maambukizi yakiwa kwenye figo huweza kusababisha maumivu makali zaidi.
Dalili Za Ugonjwa Wa UTI
Ugonjwa wa UTI huwa na dalili zifuatazo,japo si mara zote huonesha dalili:
-Hamu kubwa ya kukojoa isiyoisha
-Maumivu yanayochoma wakati unakojoa
-Kukojoa kiasi kidogo cha mkojo mara kwa mara
-Mkojo kuwa na rangi ya kola au chai
-Mkojo wenye damu
-Mkojo kunuka sana
-Maumivu makali chini ya kitovu hasa kwa wanawake
-Maumivu ya misuli na tumbo
-Kichefuchefu na kutapika
-Homa
Chanzo Cha Ugonjwa Wa UTI
Maambukizi kwenye njia ya mkojo husababishwa kwa sehemu kubwa na baktria wanaoitwa Escherichia coli (E.coli) wanaopatikana kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Hawa husababisha maambukizi kwenye kibofu cha mkojo. Bakteria wengine ni chlamydia na mycoplasma ambao husababaisha maambukizi kwenye mirija ya urethra.
Magonjwa ya UTI hupewa majina kulingana na mahali inapotokea:
Cystitis-ni ugonjwa wa maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
Urethritis-ni maambukizi ya maambukizi kwenye mirija ya urethra
Pyelonephritis-ni ugojwa wa maambukizi kwenye figo
Maambukizi kwenye mirija ya ureta ni adimu sana.
Sababu Hatarishi Za Kupata Ugonjwa Wa UTI
Watu wa jinsi na umri wote wanaweza kupata ugonjwa wa UTI,japo wengine huwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa kuliko wengine. Sababu zifuatazo huweza kuongeza uwezekano wako kupata maambukizi ya njia ya mkojo:
-Kuwa mgonjwa wa kisukari
-Usafi binafsi duni
-Kuwa na matatizo ya tezi dume
-Kuwekewa mpira wa mkojo
-Kibofu cha mkojo kubaki na mkojo mara nyingi
-Tatizo la kushindwa kuzuia kinyesi
-Mawe kwenye figo
-Kudhoofika kwa kinga za mwili
-Kufanyiwa upasuaji kwenye njia ya mkojo
-Mazoea ya kukaa na mkojo muda mrefu bila kukojoa
-Kutumia madawa ya antibiotic kwa wingi
Kwa Nini Wanawake Wanapata UTI sana?
Maumbile ya kike-wanawake wana mirija mifupi sana ya urethra (mirija inayotoka kwenye kibofu cha mkojo hadi ukeni),jambo linalofanya bakteria wanaosababisha UTI kusafiri kwa muda mfupi tu kufika kwenye kibofu cha mkojo
Matumizi ya dawa za kuzuia mimba-wanawake wanaotumia dawa za kuzuia mimba wana hatari kubwa ya kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo. Dawa hizo ni kama:
- Spermicide-Huua mbegu za kiume,huingizwa ukeni kabla ya tendo la ndoa. Huongeza hatari ya bakteria kuingia ukeni
-Kondomu-kama hazina maji maji ya kutosha husababisha msuguano mkubwa na hivyo kuongeza hatari ya UTI
-Diaphrams-huingizwa ukeni kabla ya tendo la ndoa kuanza,ili zizuie mbegu za kiume kuingia. Pia huongeza hatari ya bakteria kuingia au kuzaliana ukeni.
Kukoma hedhi-wanawake wanapokoma hedhi,mzunguko wa homoni ya estrogen pia hukoma. Hii husababisha mabadiliko kwenye mfumo wa mkojo,na kufanya iwe rahisi kupata maambukizi.
Kufanya ngono kwa wingi-wanawake wanapokuwa katika hali ya kufanya ngono mara kwa mara na watu tofauti tofauti,huwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa UTI.
Madhara ya Ugonjwa Wa UTI
Mgonjwa akipata tiba sahihi kwa wakati sahihi,maambukizi ya njia ya mkojo sehemu za chini yaani kwenye kibofu na urethra,ni nadra sana kusababisha madhara makubwa. Lakini kama hutapata tiba sahihi na kwa wakati,maambukizi ya njia ya mkojo,huweza kusababisha madhara makubwa:
-Maambukizi ya mara kwa mara,hasa kwa wanawake ambao hupata maambukizi mara mbili au zaidi ndani ya kipindi cha miezi 6 au minne au zaidi.
-Figo kuharibika kabisa kutokana na maambukizi ya kudumu kwenye figo
-Kuzaa mtoto aliyepungua uzito,au mtoto njiti kwa akina mama wajawazito
-Mirija ya urethra kuwa myembamba kwa wanaume
-Kinga za mwili kushambulia mwili kwa sababu ya maambukizi (sepsis)
Kuzuia Ugonjwa Wa UTI
Unaweza kufanya yafuatayo,kupunguza hatari ya kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo:
Kunywa maji ya kutosha- maji yatasaidia kuyeyusha mkojo,ili ukojoe mara kwa mara. Hii itasaidia bakteria kuondolewa kwa haraka kabla hawajaanza kusababisha maambukizi
Nawa vizuri-kwa wanawake wanaoasha sehemu zao nyeti kutokea mbele kwenda nyuma huepusha hatari ya baktria kuingia ukeni kutoka njia ya kutolea kinyesi
Epuka kutumia marashi sehemu nyeti-si vyema kutumia marashi na vipodozi mbali mbali sehemu za uke kwa sababu kuleta madhara kwenye urethra na kupelekea maambukizi
Tumia njia salama za uzazi wa mpango-kuingiza chochote ukeni,zikiwemo kondomu na nyinginezo huweza kupalilia ukuaji wa bakteria wasababishao maambukizi.
Kojoa kila inapobidi-epuka kukaa na mkojo kwa muda mrefu. Pia ukimaliza tu kufanya mapenzi nenda ukojoe pia. Hii itaondoa mazingira wezeshi kwa bakteria kukua na kuzaliana.
Epuka pombe na caffeine kwa sababu huharibu kibofu cha mkojo
Hakikisha sehemu nyeti zako ni safi kabisa muda wote
Vaa nguo za pamba na zinazoachia mwili ili kulifanya eneo linalozunguka urethra kuwa kavu kabisa
Ndugu msomaji wangu leo tumeufahamu ugonjwa wa UTI kwa kina. Unasumbuliwa na UTI sugu na zisizopona mara kwa mara? Tunayo dawa kwa ajili ya UTI sugu. Tumia hii itakusaidia sana. Tuandikie kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959 kupata oda yako.
Katika mada inayokuja tutalitazama tatizo la maambukizi kwenye figo na jinsi unavyoweza kupata tiba yake. Endelea kuwa nasi. Kwa maoni,ushauri na maswali usisite kutuandia afyagreen@gmail.com wakati wowote.