Kazi Na Faida Za Ginkgo Biloba
-Kuua makali ya radikali huru na kuondoa madhara yatokanayo na kuzeeka kwa viungo
-Kuongeza uwasilishaji wa oksijeni kwenye ubongo na kuongeza kumbukumbu
-Kuzuia kudhoofika kwa macula kunakotokana na uzee
-Kuzuia au kuponya matatizo ya maumivu ya miguu (intermittent claudication)
Yafaa Kwa:
-Watu wenye tatizo la kukosa kumbukumbu
-Watu wenye ugonjwa wa Alzheimer's na/au dementia
-Watu wa umri mkubwa wanaotaka kuzuia magonjwa ya macula na kudhoofika kwa ubongo yanayoambatana na umri
-Watu wenye maumivu ya miguu yatokanayo na kukosa mzunguko mzuri wa damu
-Watu wenye umri mkubwa wanaotaka kuboresha kumbukumbu
Viungo:
Ginkgo biloba leaf extract.
Maelezo Muhimu:
Antioxidant Yenye Nguvu:
Majani ya ginkgo yana kemikali za aina mbili - flavonoids na terpenoids, ambazo zina tabia za antioxidants zenye nguvu. Antioxidants ni vitu vinavyoondoa radikali huru - michanganyiko ndani ya mwili inayoharibu ngozi laini inayozunguka seli, kuvuruga DNA, na hata kusababisha kufa kwa seli. Radikali huru zinaaminika kuchangia kwenye matatizo ya kiafya ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo na kansa na hata ugonjwa wa Alzheimer's na aina nyingine za dementia. Antioxidants kama hizo zinazopatikana ndani ya ginkgo huua makali ya radikali huru na kuweza kupunguza au kuzuia baadhi ya madhara yanayoweza kutokea.
Jani La Ubongo:
Watu wengi huiita ginkgo jani la ubongo "brain herb", ambalo limeonyesha kuboresha utendaji kazi wa ubongo. Ubongo hutumia asilimia 20 ya oksijeni ya mwili. Kwa sababu ginkgo husaidia mzunguko wa damu katika ubongo, kwa kupeleka oksijeni kwa haraka zaidi na kiufanisi. Faida ni nyingi, kama kutoa tiba ya mfadhaiko (depression) na kuongeza kumbukumbu, matendo hisia (Reflexes), na ufanyaji kazi wa ubongo kwa ujumla. Utafiti wa karibuni umeonyesha kuwa inaweza kupunguza madhara ya dementia kwa wagonjwa wenye Alzheimer's, na kufungua njia ya tiba ya aina mpya ya ugonjwa huu ulioenea na usioeleweka vizuri.Kudhoofika Kwa Macula:
Flavonoids zinazopatikana ndani ya ginkgo zinaweza kusaidia katika kuzuia au kupunguza baadhi ya matatizo ya retina - matatizo ya eneo lenye rangi nyeusi la jicho. Kudhoofika kwa macula, ambako mara nyingi huitwa age-related macular degeneration au ARMD, ni ugonjwa wa jicho ambao unaathiri retina. Ni ugonjwa unaokua, wa kudhoofisha jicho ambao una tabia ya kuathiri zaidi watu wenye umri mkubwa na ni sababu kubwa ya upofu kwa wazee.Maumivu Ya Miguu:
Kwa sababu ginkgo inaboresha mzunguko wa damu, ilifanyiwa utafiti kwa watu wenye ugonjwa wa kupata maumivu ya miguu yanayosababishwa na upungufu wa mmzunguko wa damu miguuni - intermittent claudication. Watu wenye tatizo hili wanapata shida sana kutembea kwa sababu ya kusikia maumivu makubwa. Uchunguzi kwa watu wanane ulidhihirisha kuwa kutumia ginkgo kuliongeza umbali wa kutembea kwa mita 34 ukilinganisha na wale waliotumia placebo. Kwa hiyo, ginkgo imeonyesha kuwa ni dawa ya kuitumia kwa kuongeza umbali wa kutembea bila maumivu.Nunua Ginkgo Biloba Hapa: