Kazi Na Faida Za Zinc
-Ni muhimu kwa ajili ya nishati na utendaji kazi wa mwili
-Huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa protein na utendaji kazi wa chembe hai nyekundu na nyeupe za damu
-Huongeza kinga ya mwili na kuharakisha kupona vidonda
-Husaidia mfumo wa uzazi kwa mwanaume na mwanamke
-Husaidia kuondoa ugumba
Hufaa kwa:
-Watu walio na upungufu wa zinc katika mlo wao wa kila siku
-Watu wenye matatizo ya mmeng'enyo wa chakula na acid tumboni
-Watu wanaotumia dawa kwa muda mrefu
-Watu wanaovuta sigara ama kunywa pombe kwa muda mrefu
-Watu wanaokula mboga mboga tu (vegeteranians)
-Wanawake wanaomeza dawa za uzazi wa mpango au wanaopandikiziwa homoni
-Wanariadha ama watu wa mazoezi
-Watoto
Maelezo Muhimu
Kuhusu Zinc
Zinc ni kirutubisho muhimu sana kwa ajili ya afya ya binadamu na upungufu kidogo tu wa zinc husababisha athari kubwa.Zinc ni muhimu kwa sababu hupatikana karibu katika kila tishu ndani ya mwili na huhusika moja kwa moja kwenye mgawanyo wa seli (cell division). Zinc ni antioxidant yenye nguvu sana,husaidia kuzuia kansa,lakini pia huhusika moja kwa moja kwenye utendaji kazi bora wa mfumo wa homoni (endocrine) na kuimarisha kiwango cha homoni.
Upungufu Wa Zinc
Upungufu wa zinc kwa wanaume na wanawake husababisha ugumba na kupungua kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa. Upungufu wa zinc pia huongeza athari za msongo na kuharakisha kuzeeka mapema. Upungufu wa zinc hubadili namna ya kusikia ladha na kusababisha kupenda chumvi nyingi na chakula chenye utamu.Huweza pia kusababisha kuhara,upungufu wa nishati,uchovu wa kudumu,ugumba,kinga dhaifu,kumbukumbu hafifu,kushindwa kutuliza mawazo,vidonda kuchelewa kupona,neva kushindwa kufanya kazi vizuri na kusikia sauti ya kuunguruma masikioni.
Zinc Kwa Ajili Ya Afya Ya Uzazi Kwa Mwanaume
Zinc ni madini muhimu sana kwa ajili ya kuongeza na kuimarisha kiwango cha homoni ya testesterone,na seli za tezi dume huhitaji kiwango cha zinc mara 10 zaidi kuliko seli nyingine zozote mwlini ili kufanya kazi kwa kiwango cha juu na kuwa na afya. Upungufu wa zinc kwa wanaume huharibu utengenezwaji wa homoni ya testesterone,huwaweka katika hatari ya kupata kansa ya tezi dume na huweza kusababisha ugumba. Lakini pia upungufu wa zinc husababisha kukosa hamu ya tendo la ndoa.
Zinc Kwa Ajili Ya Afya Ya Uzazi Kwa Wanawake
Kwa wanawake huchangia katika mchakato wa kukua kwa mayai (oocytes or eggs). Kama zinc itapungua kwa wanawake,yai halitakomaa vema kiasi cha kutosha kuliachia (ovulation) na kusababisha ugumba. Kiwango kizuri cha zinc huusaidia mwili wa mwanamke kutumia homoni za oestrogen na progesterone kwa ufasaha.
Huimarisha Mfumo Wa Kinga
Upungufu wa zinc kwa bahati mbaya huathiri mfumo wa kinga kwa sababu husababisha kushuka kwa utendaji wa T cell moja kwa moja na kwa haraka ajabu. Seli za T (T cell) huinua kinga ya mwili palemwili unapovamiwa na virusi,bacteria au kupata changamoto yoyote ya afya inapojitokeza. Watu wenye umri mkubwa huwa katika hatari kubwa ya upungufu wa zinc,na si mara zote husababishwa ulaji hafifu. Kuna ushahidi wa kutosha kuwa upungufu wa zinc huongezeka kwa kadri umri unavyozidi,kuzuia maambukizi,kuimarisha mfumo wa kinga na kuimarisha ufanyaji kazi wa seli.
Hulinda Mfumo Wa Mishipa Ya Moyo
Zinc hulinda mishipa ya moyo na endoepithelium. Endoepithelium ni tabaka jembamba linalotanda ndani ya mishipa ya damu na ksaidia katika mzunguko wa damu kwenye mishipa. Upungufu wa zinc huweza kusababisha upungufu kwenye kizuizi cha endothelia na kusababisha cholestrol nyingi kugandamana kwenye kuta za mishipa ya moyo. Cholestrol huongeza hatari ya magonjwa ya moyo.
Huzuia Kisukari
Zinc hutakiw akwa ajili ya kufanyaji kazi wa homoni ikiwemo insulin. Zinc hufungamana na insulini na kufanya kiwango kikubwa cha insulin kutunzwa kwenye kongosho,na kuachiwa kuingia kwenye mishipa ya damu pale tu kunapokuwa na sukari kwenye damu. Pia zinc husadia insulin kuungana na seli na kufungua mlango ili glucose iingie. Kama seli zitakataa kufunguka glucose itabakia kwenye damu na kusababisha ongezeko la sukari kwenye damu. Kiwango cha zinc kinapopungua,huwa na upungufu katika umiminwaji wa insulin,mishipa ya neva kuwa na sukari na likidumu kwa muda mrefu husababisha kisukari.
Ni Antioxidant Yenye Nguvu
Ni antioxidant bora ambayo huondoa radikali huru zinazoharibu seli za mwili kwa kuungana nazo na kuzihafifisha zisiwe na madhara. Zinc huondoa radikali huru zinazosababisha uvimbe ,na huondoa metali nzito zinazoharibu ubongo.
Uwezo Wa Kuondoa Sumu Mwilini
Metali nzito zinazojijenga kwenye seli za ubongo huweza kusababisha uhafifu wa kusafirisha taarifa kati ya neurone na ugonjwa wa Alzheimer's. Zinc huweza kuondoa sumu hizi na huweza kuimarisha hali ya afya ya ubongo.
Zinc huchangia katika usafirishaji wa taarifa baina ya neva na husaidia kuimarisha afya na umbo la ubongo. Zinc pia ni sehemu ya kimeng'enya (enzyme) ambayo husaidia kuondoa mafuta kwenye gozi nyembamba ya ubongo. Hii ni muhimu sana kwa sababu,ili kuimarisha afya na utendaji wa ubongo,ngozi hii nyembamba inapaswa kupata virutubisho vinavyotakiwa.
Huzuia Kansa
Ananda Prasad,mtafiti anaeongoza katika eneo la afya na zinc,anadokeza kuwa kudumisha kiwango bora cha zinc,inaweza kutibu matatizo mengi ya kiafya,hususani kansa na upungufu wa kinga ya mwili. Utafiti wa hivi karibuni umebaini kuwa upungufu wa zinc unahusiana moja kwa moja na kansa ya matiti,utumbo mpana,ovari,mapafu,ngozi na leukemia.
Tunataka Kiasi Gani Cha Zinc Kila Siku?
Zinc ablet for Adults
Viungo: Zinc Lactate (4mg of zinc per tablet)
Zinc Tablet for Children
Viungo: Zinc Lactate (4 mg of zinc per tablet)
Nunua Zinc Sasa: