Kazi Na Faida Za Protein Powder
.Huwezesha ukuaji na maendeleo ya mwili
.Hufanya kazi zinazoratibiwa na taarifa kutoka kwenye vinasaba (genes)
.Huunda vimenyenyo (enzymes) zinazomeng'enya chakula
.Huhusika kwenye mawasiliano ya seli
Hufaa kwa:
.Watu wenye unyafuzi kama vile walevi
.Watu waliodhoofishwa na magonjwa kama UKIMWI,kansa,kifua kikuu,kisukari n.k
.Watu wanaokula mboga tu (vegeterians) wenye upungufu wa protein
.Wanariadha wenye kusudi la kujenga misuli
.Watu walio katika mpango wa kupunguza uzito
Maelezo muhimu
Umuhimu Wa Protein
Protein ni kirutubisho muhimu sana katika maisha yetu. Kazi za mwili kama vile utendaji kazi wa mwili (metabolism),ukuaji wa mifupa,utengenezwaji wa viungo,kufanywa upya kwa tishu za mwili na uongezwaji wa nishati,haziwezi kufanyika bila kuwepo kwa protein. Ukuaji na maendeleo ya mwili,kupona kwa tishu zilizojeruhiwa,utendaji kazi wa mwili (metabolism),utengenezwaji wa vimeng'enyo (enzymes),mfumo wa kinga ya mwili,kuimarishwa mwili na kupunguza kuzeeka haraka na kuongeza siku,yote hayawezi kufanyika bila protein.
Upungufu Wa Protein
Upungufu wa protein katika mwili wa binadamu husababisha mwili kushindwa kufanya kazi zake vizuri,kuanza kupoteza kumbukumbu na mengineyo kama kupoteza ubora wa ngozi,misuli kuwa dhaifu, na inaweza kusababisha magonjwa mengine pia.
Tunahitaji Protein Kiasi Gani?
Mahitaji yetu ya protein huendana na umri,ukubwa wa mwili na kazi unazofanya. Njia bora ambayo hutumiw ana watalaam wa lishe kuweza kukadria kiwango cha chini cha protein unachohitaji kwa siku,ni kuzidisha uzito wa mwili katika kilogram kwa 0.8 au uzito wa mwili katika pounds kwa 0.37. Hiki ndich okiwango cha chini katika gram cha protein anayopaswa mtu kupata kwa siku. Kwa mfano mtu mwenye uzito wa kilo 60 anapaswa kula gram 28 za protein kwa siku.
Tahadhali:
Watu walio na matatizo makubwa ya ini na figo wanapaswa kuzuia matumizi ya protein. Kwa hiyo bidhaa hii haishauriwi kutumiwa na mtu mwenye matatizo ya ini au kushindwa kwa fugo (kidney failure)