Karibu ndugu msomaji katika tovuti yetu,AFYA YAKO, KIPATO CHAKO. Katika tovuti hii tumeelezea kwa uwazi na ufasaha namna unavyoweza kuboresha na kuimarisha afya yako. Wapo watu wanaotafuta kwa hali n amali kuweka afya zao mahali pake lakini imekuwa mtihani kwa sababu kadha wa kadha. Katikika tovuti hii utakutana na bidhaa bora kabisa na zilizo muhimu kwelkweli katika uimarishaji wa afya yako. Nikupongeze kutembelea tovuti hii na endelea kuwa nasi.
Afya Ni Nini?
Kulingana na Shirika la Afya Duniani, Afya ni haki ya kuwa vizuri kimwili,kiakili na kijamii. Kuwa na afya siyo tu kukosa magonjwa kabisa bali pia ni uwezo wa kuondokana na magonjwa na matatizo mengineyo. Afya ya binadamu hutambuliwa kwa mambo mbalimbali kama vile vinasaba,mazingira,mahusiano na elimu. Wakati lishe bora,mazoezi,kupima na kutafuta ufumbuzi wa magonjwa mbali mbali huweza kuchangia kuimarisha afya yako.
Jinsi Ya Kuimarisha Afya Yako
Watalaamu na washauri wengi wa afya wana mambo mengi wanayoshauri juu ya uimarishwaji na uendelezwaji wa afya katika ubora wake. Lakini kwa ujumla wake wote hukubaliana kuwa baadhi ya mambo yafutayo husaidia kuimarisha afya yako ukiyazingatia:
Maji-Kunywa maji angalau lita 2 (glasi 8) kwa siku na kuyatumia maji nje ya mwili kuoga kila siku husaidia kuondoa sumu mwilini na kuimarisha afya yako
Mazoezi-Kufanya mazoezi angalau ya kutembea kilomita 8 kwa siku huwa na mchango bora wa kuimarisha afya yako
Mwanga wa jua ambao husaidia kutengeneza madini yanayoimarisha mifupa
Lishe Bora-inashauriwa kuwa na asilimia kubwa inayotokana na mimea husadikika kuwa na virutubishi vinavyousitahili mwili.
Greenworld Na Afya Yako
Greenworld ni watengenezaji wa bidhaa lishe na tiba zitokanazo na mimea asilia kabisa. Bidhaa hizi toka greenworld hazitokani na kemikali kabisa bali zimetengenezwa na mimea pekee. Lakini pia bidhaa hizi zinakuwa muhimu sana kwa jamii kwa sababu hushughulika na chanzo cha tatizo.Sasa kama una tatizo lolote lenye chanzo bainishi,hizi ni bidhaa muhimu kwa ajili yako.
Katika tovuti hii tutatazama kwa kina juu ya bidhaa hizi,tutafahamu umuhimu wake,manufaa yake na jinsi kutibu matatizo kadha wa kadha kwa kutumia dawa hizi. Kama umekuwa ukitafuta dawa za asili kwa ajili ya afya yako,hapa umefika penyewe,zipo tele kwa ajili yako.
Karibu sana..