Leo tunatazama ugonjwa mwingine wa figo wa kuharibika kwa vichujio vya figo(gomeruli). Huu ni mkusanyiko wa magonjwa yote yanayodhuru sehemu ya figo inayohusika na kuchuja damu. Sehemu hii inaitwa glomeruli. Glomerulonephritis pia huitwa nephritis. Figo zinapodhurika hushindwa kuchuja uchafu na maji yaliyozidi mwilini. Kama magonjwa yataendelea husababisha figo zishindwe kufanya kazi kabisa na kupelekea ugonjwa sugu wa figo.
Vichujio hivi huondoa uchafu na maji yaliyozidi mwilini na kuondoa nje ya mwili kwa njia ya mkojo.
Dalili Za Ugonjwa Wa Glomerulonephritis
Baadhi ya dalili ambazo huonekana kwa mtu mwenye ugonjwa wa kuharibika vichujio vya figo, ni kama zifuatazo:
-Kuvimba uso
-Kupungua kiwango cha mkojo
-Kukojoa mkojo wenye damu
-Maji kwenye mapafu,yanayopelekea kukohoa
-Shinikizo la juu la damu
-Kukojoa mara kwa mara usiku
-Kukojoa mkojo mweusi kwa sababu ya uwingi wa protini
-Maumivu ya tumbo
-Kutokwa damu puani mara kwa mara
-Kuvimba miguu,mikono na tumbo
Chanzo Cha Ugonjwa Wa Glomerulonephritis (GN)
Ugonjwa wa kuharibika kwa vichujio vya figo huweza kusababishwa na:
1. Maambukizi
-Maambukizi kwenye koo na ngozi
-Bacterial endocarditis-ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria walioingia kwenye mkondo wa damu,na kukaa kwenye kuta za moyo,vyumba vya moyo au kwenye mishipa ya damu.
-Maambukizi ya virusi-maambukizi ya virusi kama VVU,virusi vya hepatitis B na C huweza kusababisha vichujio vya figo kuharibika
2. Magonjwa ya kinga
-Lupus-hutokea pale kinga za mwili zinaposhambulia tishu na viungo vya mwili. Huweza kushambulia ngozi,joints,figo,moyo,seli za damu na mapafu.
-Goodpasture syndrome-hutokea pale mfumo wa kinga unaposhambulia figo na mapafu. Hushambulia protini inayopatikana kwenye mapafu na figo
-IgA nephropathy-ni ugonjwa unaotokana na kinga za Immunoglobin A kujijenga kwenye glomeruli.
3. Magonjwa yanayodhuru mishipa ya damu
-Polyarteritis-ni ugonjwa adimu sana unaotokana na kudhurika kwa mishipa ya damu kunakopelekea viungo kama moyo,neva na utumbo mwembamba na joints.
-Ugonjwa wa mishipa ya damu unaodhuru mishipa midogo ya damu kwenye mapafu na figo.
4. Magonjwa yanayodhuru Glomeruli moja kwa moja
-Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu
-Ugonjwa wa kisukari wa figo
Ugonjwa wa glomerulonephitis huweza pia kurithiwa katika familia. Lakini pia huweza kusababishwa na aina fulani za kansa kama vile kansa ya mapafu na nyinginezo.
Madhara Ya Kuharibika Kwa Vichujio Vya Figo
Vichujio vya figo vikiharibika,huweza kusababisha mgonjwa kupata:
-Acute kidney failure-Ugonjwa wa figo kushindwa ghafula
-Chronic kidney failure-Ugonjwa sugu wa figo
-High blood pressure-Shinikizo la juu la damu
-Nephrotic syndrome-ugonjwa unaosababisha mwili kuvimba.
Jinsi Ya Kujikinga Na Ugonjwa Wa Kuharibika Kwa Vichujio Vya Figo
-Pata tiba ya maambukizi yako mapema kuepusha madhara zaidi
-Fanya ngono salama kuepuka maambukizi ya virusi
-Dhibiti na kutibu ugonjwa wa shinikizo la damu
-Dhibiti na kutibu ugonjwa wa kisukari
Huu ni Ugonjwa wa kuharibika vichujio vya figo (glomeruli). Lakini tumegundua kwamba magonjwa mbali mbali ndiyo yanayochangia mtu kupata ugonjwa huu wa glomerulonephritis. Mada itakayofuata tutatazama ugonjwa mwingine wa figo-ugonjwa wa figo unaosababisha mwili kuvimba.
Kama unasumbuliwa na ugonjwa huu wa figo-kudhurika kwa vichujio vya figo,basi usisite kumwona daktari. Lakini pia unaweza kuwasiliana nasi muda wowote kupata virutubisho bora vitakavyoimarisha figo zako na kukukinga na maradhi mbali mbali ya figo.
Wasiliana nasi kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie kupitia +255 673 923 959 kupata dawa zetu za asili zitakazokusaidia kuondoa chanzo cha tatizo lako.
Kwa maoni au ushauri,tuandikie pia kupitia afyagreen@gmail.com.