Ini ni kiungo chenye ukubwa wa mpira wa miguu kilichofunukwa na mbavu upande wa kulia wa tumbo lako. Ini husaidia kumenyeng'enya chakula,na kuondoa sumu mwilini. Ugonjwa wa figo huweza kurithiwa au kusababishwa na mambo kadha wa kadha ikiwemo maambukizi ya virusi na unywaji pombe. Pia uzito kupita kiasi huhusiana moja kwa moja na magonjwa ya ini.
Athari za muda mrefu kwenye ini husababisha makovu kwenye ini (cirrhosis) ambayo hupelekea tatizo hatarishi kabisa la ini kufeli.
Dalili Za Ugonjwa Wa Ini
Homa ya manjano-macho na ngozi kuwa njano
-Maumivu ya tumbo na kuvimba
-Kuvimba miguu na vifundo vya miguu
-Ngozi kuwasha
-Mkojo kuwa na rangi nyeusi
-Kujisaidia kinyesi chenye rangi ya udongo
-Uchovu sugu
-Kichefuchefu na kutapika
-Kupoteza hamu ya kula
-Hali ya kuvilia damu kwa haraka
Chanzo Cha Ugonjwa Wa Ini
Ugonjwa wa ini una husababishwa na mabo kadha wa kadha,kama yafuatayo:
1. Maambukizi
Vimelea vya magonjwa (parasite) na virusi husababisha maambukizi kwenye ini na kusababisha udhaifu wa kiutendaji.Virusi wanaosababisha maambukizi kwenye ini huenea kupitia mkondo wa damu,manii,chakula na maji machafu,kugusana na mtu mwenye maambukizi.
Maambukizi mengi ya ini ni yale ya virusi wa hepatitis,kama:
-Hepatitis A
-Hepatitis B
-Hepatitis C
2. Mvuruguiko wa mfumo wa kinga
Magonjwa ambayo kinga za mwili hushambulia eneo fulani la mwili (autoimmune) huweza kuathiri ini. Magonjwa ya kinga kushambulia ini (autoimmune liver diseases) ni:
-Hemochromatosis
-Hyperoxaluria na oxalosis
-Wilson's disease
-Alpha-1 antitrypsin deficiency
3. Kansa na vimbe mbalimbali
Magonjwa haya ni kama:
-Kansa ya ini
-Kansa ya mrija wa nyongo
-Liver adenoma
4. Matatizo mengineyo
Matatizo mengine yanayosababisha kupata ugonjwa wa ini ni kama:
-Unywaji sugu wa pombe
-Mrundikano wa mafuta kwenye ini
Sababu Hatarishi Za Ugonjwa Wa Ini
Mambo yanayoweza kukuweka katika hatari ya kupata ugonjw awa ini ni:
-Kunywa pombe kupita kiasi
-Kuchangia sindano na vitu vyenye nca kali
-Kuchora tatoo na kujitoboa mwili
-Kugusa damu na maji maji ya watu wengine
-Ngono isiyo sa,ama
-Kujiweka katika mazingira ya kufikiwa na kemikali na sumu mbali mbali
-Kuwa na kisukari
-Uzito kupita kiasi
Kujikinga Na Ugonjwa Wa Ini
Madhara ya ugonjwa wa ini hutegemea na chanzo cha ugonjwa huo. Ugonjwa wa ini usipotibiwa hupelekea ini kufeli,tatizo hatarishi kabisa katika maisha. Unaweza kufanya yafuatayo kujikinga na ugonjwa wa ini:
Usinywe pombe kupita kiasi-pombe ni chanzo kikuu cha athari za ini.
Epuka tabia hatarishi-kuwa makini,epuka matumizi ya vitu vyenye ncha kali,na pia epuka ngono zembe.
Pata chanjo-kama uko katika hatari ya maambukizi ya ini,au kama umewahi kupata maambukizi ya hepatitis, ni muhimu kupata chanjo ya hepatitis A na B.
Tumia dawa kwa umakini-Hii itakusaidia kupunguza sumu kwenye ini lako.
Epuka kushika damu au majimaji ya watu wengine-ni kwa sababu virusi wa hepatitis husambaa na kuenezwa kwa njia hiyo
Chukua tahadhari unapopulizia dawa-dawa hizi zinaweza kusababisha maambukizi kweny ngozi na viungo vyako
Linda ngozi yako-iweke ngozi yako katika mazingira ambayo haiwezi kuingiliwa na kemilali na maambukizi kwa wepesi
Dumisha uzito bora-uzito kupita kiasi husababisha ini lako kujaa mafuta
Hapa tulikuwa tunatazama ugonjwa wa ini,endelea kuwa nasi tunapoendelea kujadili magonjwa mengine ya ini. Fuatilia mada ijayo tutakapotazama ugonjwa wa mafuta kwenye ini.
Kwa maoni,ushauri au maswali,tafadhali wasiliana nasi kupitia afaygreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.