UGONJWA WA INI KUHARIBIKA-LIVER CIRRHOSIS

Liver cirrhosis ni ugonjwa wa ini kuharibika. Ni hali ya kuongezeka taratibu kwa tishu zenye makovu kwenye ini badala ya tishu zenye afy... thumbnail 1 summary


Liver cirrhosis ni ugonjwa wa ini kuharibika. Ni hali ya kuongezeka taratibu kwa tishu zenye makovu kwenye ini badala ya tishu zenye afya. Ni ugonjwa endelevu,unaodumu kuongezeka taratibu baada ya miaka kadhaa. Kama ukiachwa uendelee,kujengeka kwa tishu zenye makovu kwenye ini huweza kuharibu utendaji kazi wa ini.

Cirrhosis hutokea kwa sababu ya uharibifu wa muda mrefu na endelevu wa ini. Tishu zenye afya za ini zinapodhurika na badala yake zikajazana tishu zenye makovu au zilizodhurika na kuharibika,tatizo hutokea. Tatizo hili huweza kuwa hatarishi zaidi kwa sababu huziba mirija ya damu na kuzuia damu kumiminika kwenye ini.

Tatizo la ini kuharibika haliwezi kutibika katika hatua za mwisho,lakini kama ugonjwa huu wa ini utagundulika mapema na chanzo kikatibika,madhara zaidi huzuiwa na kiasi fulani tatizo hupungua au kutibika.


Dalili Za Ugonjwa Wa Ini Kuharibika



Ini kuharibika hakuna dalili kabisa,ila katika hatua za baadaye zaidi,huonesha dalili zifuatazo:

-Uchovu

-Kutokwa kwa urahisi

-Damu kuvilia kwa urahisi

-Ngozi kuwasha

-Njano-macho,ngozi na mkojo

-Tumbo kujaa maji

-Kupoteza hamu ya kula

-Kichefuchefu

-Kuvimba miguu

-Kupungua uzito bila kupanga

-Kukosa utulivu

-Mishipa ya damu kuwa na mpangilio wa buibui

-Viganja vya mikono kuwa na wekundu

-Maziwa kuwa makubwa kwa wanaume

-Kupoteza kumbukumbu

-Nywele kunyonyoka

-Kupoteza hamu ya tendo la ndoa

-Damu kutoka puani

-Kushindwa kupumua vizuri

-Maumivu bega la kulia

-Kutapika damu


Chanzo Cha Ini Kuharibika



Sababu kuu za ini kuharibika ni:

-Unywaji sugu wa pombe

-Maambukizi sugu ya virusi wanaosababisha hepatitis b na c

-Mrundikano wa mafuta kwenye ini-yasiyosababishwa na pombe(Nao alcoholic fatty liver)


Sababu Zingine Za Ugonjwa Wa Ini Kushindwa ni kama:


-Chuma kujijenga mwilini (hemochromatosis)

-Shaba kugandamana mwilini

-Matatizo ya kinasaba ya mmeng'enyo wa chakula

-Autoimmune hepatitis

-Kuharibika kwa mirija ya nyongo

-Kuharibika kw amfuko wa nyongo

-Maambukizi kama vile kaswende

-Madawa kama methotrexate


MadharaYa Ini Kuharibika



Madhara yanayohusiana na mtiririko wa damu:

Portal Hypertension-ni msukumo wa damu kwenye mishipa ya vena inayopeleka damu kwenye ini. Cirrhosis huzuia mtiririko wa damu kwenye ini,na kuongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya portal ya ini

Kuvimba miguu na tumbo-Presha ya mishipa ya portal,husababisha maji kujikusanya miguuni na tumboni.

Wengu (spleen) kuvimba-portal hypertension husababisha mabadiliko kwenye wengu.

Kutokwa damu-presha kwenye mishipa ya portal husababisha damu kurejeshwa kwenye mirija midogo na kusababisha iwe mikubwa kuliko kawaida yake. Hii husababisha mishipa kupasuka na damu kuchuruzika.

Madhara Mengine:


Maambukizi-ukipata cirrhosis,mwili wako huwa katika hatari ya kushindwa kupambana na maambukizi

Utapiamlo-cirrhosis huzuia mmeng'enyo bora wa chakula na kusababisha mwili kuwa dhaifu na kupungua uzito

Sumu kwenye ubongo (hepatic encephalopathy)-ini likiharibika,hushindwa kuondoa sumu kwenye mishipa ya damu mwilini. Hii husababisha sumu kujijenga kwenye ubongo na kusababisha upoteze utulivu na kuchanganyikiwa.

Njano-hutokana na ini kushindwa kuondoa uchafu wa bilirubin,unaotokana na kuvunjwa vunjwa kwa seli nyekundu za damu. Billirubin ikigandamana husababisha njano kwenye macho,mikono n.k

Magonjwa ya mifupa-baadhi ya watu wenye ini lililoharibika hupoteza uwezo wa mifupa na kuiweka katika hatari ya kuvunjika muda wowote

Kansa ya ini-watu wengi wenye kansa ya ini huwa wana cirrhosis pia.

Ugonjwa wa ini kushindwa kufanya kazi kabisa-watu wengi wenye matatizo ya ini kushindwa huwa na matatizo ya cirrhosis.



Jinsi Ya Kujiepusha Na Ugonjwa Wa Ini Kuharibika



Ili kujiepusha na madhara ya ini kuharibika,fanya yafuatayo:

Usinywe pombe-pombe inaharibu ini moja kwa moja. Dhamiria na anza mazoezi mara moja ya kuacha pombe ili kutunza afyaya ini lako.

Kula chakula bora-kula matunda,mbogamboga na nafaka nzima kutunza ini lako

Dumisha uzito unaotakiwa-ongezeko la mafuta mengi mwilini huongeza hatari ya ugonjwa wa ini kushindwa

Punguza hatari ya hepatitis-matumizi ya vitu vyenye ncha kali huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa ini kuharibika



Tumekuwa tukiliangazia tatizo la ini kuharibika,chanzo, dalili zake pamoja na madhara uwezayo kuyapata ukiwa na tatizo hili. Hii ni hatua ya mwisho ya ini kuharibika ambayo haina tiba ya moja kwa moja,ila tu unaweza kupunguza madhara yake kama una tatizo la ini kuharibika.

Ushauri muhimu ni kuzingatia kuimarisha afya ya ini kwa kutumia chakula bora,na kutumia virutubishi tiba vinavyojenga afya ya ini,ili kuepuka madahara zaidi ya ini. Hii itakusaidia kuepuka magonjwa mbalimbali ya ini.

Kupata dawa,bofya hapa:

Kwa mahitaji ya dawa na virutubishi vya ini wasiliana nasi kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959 sasa.