Kazi na Faida zake
.Kuboresha utolewaji wa insulin na kongosho
.Kupunguza kiwango cha sukari kwa kuongeza usikivu wa mwili wa homoni ya insulin
.Kusimamia uingizaji na uvunjaji wa sukari ya mwili.
Yafaa kwa:
. Watu wenye kisukari - Type II diabetes
. Watu wenye kiwango kikubwa cha lipids
Viungo: Majani ya mulberry, astragalus, majani ya ginkgo na Balsam pear
Maelezo Muhimu
Kisukari Ni Nini?
Kisukari ni ugonjwa ambao husababisha mwili kushindwa kutengeneza au kutumia insulin na kusababisha kiwango cha sukari katika mwili kuwa juu (Hyperglycemia). Kuna aina mbili za kisukari;
1. Type I: Katika aina hii ya kisukari, seli za kuzalisha insulin ndani ya kongosho huwa zimeharibika na mwili hauwezi tena kutengeneza insulin wenyewe. Mgonjwa wa aina hii ya kisukari lazima achomwe sindano za insulin.
2. Type II: Katika aina hii ya kisukari mwili wa mgonjwa unatengeneza insulin kwa kiwango cha kutosha lakini mwili unashindwa kuipokea. Kutokana na hali hiyo, glucose haiingii ndani ya mwili na hivyo kujaa ndani ya damu. Mgonjwa mwenye tatizo hili, anatakiwa kutumia dawa za kumsaidia.
Madhara yatokanayo na kisukari
1. Kisukari kinaongoza kwa kusababisha tatizo la kutokuona (diabetic retinopathy) baina ya watu wa umri wa kufanya kazi
2. Kisukari ni chanzo nambari moja cha matatizo ya figo (diabetic nephropathy)
3.Kisukari kinaongoza kwa kusababisha kukatwa kwa viungo (diabetic neuropathy)
4. Kisukari kinasababisha mwongezeko wa vifo vinavyotokana na matatizo ya moyo na kiharusi kwa mara mbili hadi nne.
Uwingi wa sukari mwilini
Sukari iliyo ndani ya mwili hutupa nguvu ili kufanya shughuli zetu za kila siku. Kiwango cha sukari katika mwili hupanda baada ya kupata chakula. Glucose huingia kwenye seli na kushiriki kwenye mfululizo wa hatua za kikemikali kwa kuelekezwa na insulin na mwisho mwili hupata nguvu za kufanya kazi. Kukiwa na upungufu wa insulin katika mwili , au kama mwili utajijengea hali ya kukataa kuitumia insulin, insulin na glucose haviwezi kuingia kwenye seli kikawaida. Hii husababisha glucose kuwa nyingi ndani ya damu na hatimaye, kisukari.
Kisukari na madhara yake
Baada ya kisukari kutokea, kiwango kikubwa cha glucose hutolewa na mkojo. Wakati huo huo dalili nyingine huonekana, kama kunywa maji sana, kukojoa mara kwa mara, kula sana, kupungua uzito, kizunguzungu na uchovu wa mwili. Madhara makubwa huweza kutokea kwenye macho, figo, neva, ngozi, mishipa ya damu na moyo. Mwisho, upofu, kuoza kwa viungo vya chini vya mwili, kiharusi au kufa kwa seli za moyo (cardic infarction) hutokea, ambavyo huhatarisha afya ya mgonjwa kwa kiasi kikubwa sana.
Glucoblock Ya Green World inarekebishaje kiwango cha sukari?
A. Kuzifanyia ukarabati seli za beta (B-cells) na kurudisha uwezo wake wa kutengeneza insulin.
B. Inapunguza sukari katika damu, inaondoa dalili za kisukari, kurudisha utendaji kazi wa insulin, kurudishia utoaji wa seli za insulin, kurudisha usikivu wa vipokezi vya insulin.
C. Inasimamia uingizaji wa wanga, uvunjaji wa wanga na mfumo wa fahamu, inaondoa ukinzani wa mwili unaosababisha kisukari hivyo kurudisha ufanyaji kazi wa seli za insulin.
D. Kupunguza na kuzuia madhara makubwa yanayoletwa na kisukari.
E. Kusimamia kinga za mwili. Kuzuia na kupunguza maambukizi yanayotokana na uwingi wa sukari katika mwili.
Nunua Glucoblock toka Green World Tanzania: