KUHUSU GREENWORLD TANZANIA

Green world Tanzania ni tawi la Kampuni ya Green world USA yenye makao yake makuu Michigan nchini Marekani. Green world Tanzania ni ... thumbnail 1 summary






Green world Tanzania ni tawi la Kampuni ya Green world USA yenye makao yake makuu Michigan nchini Marekani. Green world Tanzania ni moja kati ya matawi zaidi ya 70 ya kampuni hii yaliyoenea duniani kote. Ni moja kati ya matawi zaidi ya 23 katika bara la Afrika. Kampuni ya Green world ilianza kuingia Afrika mnamo mwaka 2007 katika nchi ya Afrika ya kusini. Mnamo mwaka 2008 kampuni ya Green world ilisajiriwa rasmi nchini Tanzania.


Kuanzishwa Kwa Kampuni Ya Greenworld



Greenworld USA ilianzishwa mnamo mwaka wa 1994 Michigan nchini Marekani. Mwasisi wa kampuni hii ni Dr. Deming Li Mmarekani mwenye asili ya China aliyepata masomo yake nchini Marekani. Kilijengwa kituo kikubwa cha utafiti wa magonjwa mbalimbali hapo Michigan.



Mwanzilishi Wa Kampuni




Mwanzilishi wa Greenworld ni Dr. Deming Li Profesa wa masomo ya Microbiology,raia wa Marekani aliyezaliwa nchini China. Wakati akiwa kwenye masomo yake nchini Marekani alidhamiria kufanya tafiti na kugundua kuwa dawa zinazotumiwa na watu haziondoi magonjwa ila tu huondoa dalili za magonjwa. Baada ya utafiti wa muda mrefu,akaamua kuanzisha tiba za mimea ambazo zimekuwa msaada mkubwa kwa watumiaji ulimwenguni hadi sasa.



Makao Makuu Ya Green world


Makao makuu ya Greenworld yapo Michigan nchini Marekani. Pia hapo kuna kituo kikubwa cha utafiti kilichoanzishwa tangu mwaka 1994.






Bidhaa Za Green world




Bidhaa za Greenworld ni za mimea ya asili kabisa. Mashamba na viwanda vya Greenworld vinapatikana nchini China. Huko kuna viwanda vya Tianjin na Nanjing ambapo bidhaa hizi huzalishwa. Hadi sasa kuna zaidi ya aina 150 ya bidhaa za afya zinazotengenezwa na Greenworld.




Matawi Ya Green world



Tangu kuanza kwa biashara ya Greenworld mwaka 1997,imefanikiwa kuwa na matawi mengi yanayozidi kuongezeka kulingana na uhitaji wa bidhaa na biashara ya kampuni hii. Hadi sasa ina matawi 70 duniani kote,Afrika kukiwa na zaidi ya matawi 23 katika nchi mbali mbali ikiwemo na Tanzania.


Mfumo Wa Biashara Wa Green world



Greenworld ilichagua kusambaza bidhaa zake kwa njia ya Biashara ya mtandao (Network Marketing),mfumo uliosaidia kuifanya ifikie nchi nyingi kwa wakati mfupi. Mfumo wa biashara wa Greenworld unampa nafasi ya kwanza msambazaji wa bidhaa ili anufaike na hivyo ataisaidia kampuni pia kuendelea. Mfumo huu wa biashara umepata ufanisi kwa sababu ya uwingi wa bidhaa za Greenworld.


Kwa ufupi nimekuletea historia ya Greenworld,inayoonesha uanzishwaji wake na utendaji kazi wa kampunihii. Naamini umefatilia kwa umakini na umeweza kuelewa Greenworld ni nini. Endelea kufuatana nasi,katika mada zinazofuata tutatazama Kwa nini Greenworld ni sehemu sahihi kwa ajili yako,Wanachama wa Greenworld Tanzania na Mafao au Manufaa ya wanachama wa Greenworld.

Je,umegundua ni wakati mwafaka kujiunga na Greenworld? Karibu uwasiliane nasi kufikia ndoto zako na Greenworld.
Kwa maoni,ushauri au maswali tafadhali wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie 0673 923 959