Mifupa ni muhimu sana katika mwili wako. Mtu yeyote huweza kupiga hatua kwa sababu ya mpangilio wa mifupa ulio ndani ya mwili wake. Katika umri mdogo kiwango cha mifupa mipya kutengenezwa ni kikubwa sana kuliko kiwango cha mifupa inayokufa. Lakini mambo huwa kinyume katika umri mkubwa,kiwango cha mifupa kufa huwa ni kikubwa sana kuliko kiwango cha mifupa inayotengenezwa. Hii huelezea kwa nini kuna umuhimu wa kutumia virutubisho vinavyojenga mifupa katika umri mdogo na virutubisho vinavyotunza na kuhifadhi mifupa wakati wa umri mkubwa.
Magonjwa Ya Mifupa
Magonjwa yamifupa ni mengi sana lakini hapa tunaangazia kwa ufupi baadhi ya magonjwa ya mifupa. Yapo magonjwa yatokanayo na umri kuongezeka lakini pia kuna magonjwa ya mifupa katika umri mdogo.
Rickets-Ni ugonjwa wa mifupa unaosababisha mifupa ya miguu kupinda. Ni ugonjwa unaowapata watoto wengi kwa sababu ya kukosa madini ya calcium na vitamin D. Watoto wengi ndio waathrikao na ugonjwa wa matege.
Osteoporosis- Ni ugonjwa wa miifupa ambapo mifupa huwa milaini sana na kuweza kuvunjika wakati wowote. Watu wenye umri mkubwa ndio huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na ugonjwa wa osteoporosis. Mtu mwenye ugonjwa huu hupatwa na tatizo la mgongo kupinda na mara nyingi utamwona akitembea huku ameinama kwa sababu mifupa ya mgongo wake huanza kuvunjika.
Magonjwa Ya Maungio Ya Mifupa-Arthritis
Arthritis ni ugonjwa wa maungio ya mifupa ya binadamu. Ugonjwa huu hutokana na kuwepo kwa tatizo fulani katika maeneo ya maungio ya mifupa. Arthritis ni mkusanyiko wa magonjwa zaidi ya 500 yanayohusisha maungio ya mifupa. Katika kipengele hiki tutatazama aina chache hivi za magonjwa ya maungio ya mifupa.
Osteoathritis
Ni ugonjwa wa maungio ya mifupa unaotokea pale cartilage inaposagika na kupoteza ubora wake. Hali hii husababisha mifupa inayokutana kwenye maungio kusagika moja kwa moja na kusababisha maumivu makali ya mifupa. Watu wenye umri mkubwa na wenye unene mkubwa huwa katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya ugonjwa wa maungio ya mifupa. Wanawake ndio hupata ugonjwa huu zaidi kuliko wanaume.
Ugonjwa huu hushambulia zaidi mikono,magoti,nyonga,shingo na upande wa chini wa mgongo.Huambatana na maumivu makali katika joints, joints hukaza hasa unapoamka asubuhi ama baada ya kukaa kwa muda mrefu,shida katika kutembea na wakati mwingine joints huvimba na kuonekana nyekundu na zenye joto unapozigusa. Huanza taratibu lakini maumivu huongezeka kwa kadri muda unavyoongezeka.
Rheumatoid Arthritis
Aina hii ya ugonjwa wa arthritis hutokea pale kinga za mwili zinaposhambulia maungio ya mifupa. Kuna wakati kinga za mwili hushambulia sehemu fulani ya mwili tatizo linalojulikana kama Autoimmune. Kinga hizi hushambulia utando unaofunika maungio ya mifupa na kusababisha mifupa inayozungukwa na utando huo kusagika na cartilage kupoteza ubora wake kabisa.
Tofauti na osteoarthritis,rheumatoid arthritis huathirimwili wote. Madhara yake hufikia kuathiri mapafu na mfumo mzima wa upumuaji,macho,ngozi,mdomo na tezi ya mate,moyo,damu na mishipa ya damu.
Ugonjwa Wa Gout
Ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa maungio ya mifupa na kusababisha maumivu makali sana. Huwapata zaidi wanaume wenye umri wa miaka kuanzia 40-50 kuliko wanawake,japo wanawake wanapokoma hedhi huwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.
Ugonjwa wa gout hutokea kama matokeo ya kujikusanya kwa uric acid kwa wingi kwenye maungio ya mifupa. Ikumbukwe kuwa uric acid ni uchafu unaotokana na kuvunjwa vunjwa kwa chakula ain aya purine ndani ya figo na kutolewa nje. Kama uric acid itashindwa kutolewa nje hujikusanya chini ya ngozi inayozunguka maungio ya mifupa na kusababisha ugonjwa wa gout.
Magonjwa ya mifupa kama tulivyoona hapo juu,ni hatarishi hasa kwa watu wenye umri mkubwa,ambapo kiwango cha mifupa kufa ni kikubwa kuliko kiwango cha mifupa inayotengenezwa. Ugonjwa hatarishi kama Osteoporosis huweza kutibiwa na mgonjwa kupata unafuu kwa kutumia Calcium au Compound Marrow Powder,Multivitamins,Soy Power na Cordyceps.
Tiba ya mgonjwa wa Osteoarthritis ni kwa kutumia dawa ya Joint health,Calcium au
Compound Marrow Powder na Cordyceps.
Kwa mgonjwa mwenye rheumatoid arthritis atalazimika kuongeza propolis capsule ili kuleta msawazo sawia katika afya yake.
Kwa leo tutaishia hapa katika kuielezea tiba ya magonjwa ya mifupa. Unaweza kusoma zaidi kuhusu Magonjwa Ya Mifupa,Magonjwa Ya Maungio Ya Mifupa na Ugonjwa Wa Gout. Kama unasumbuliwa na tatizo lolote la mifupa na unahitaji tiba kutatua tatizo lako,wasiliana nasi kupitia 0673 923 959 wakati wowote.
Tiba Ya Magonjwa Ya Mifupa