Ugonjwa wa figo unaosababisha mwili kuvimba,husababisha mwili kupoteza protini kwa wingi. Hii hutokana na sehemu ya figo inayochuja damu kudhurika na hivyo kufanya protini ipotee moja kwa moja kwa njia ya mkojo.
Ugonjwa huu huwapata watu wa umri wowote,japo mara nyingi hutokea kwa watoto. Mgonjwa huweza kujikuta kwenye mzunguko wa kupona na kuugua tena na tena,na jambo hili huweza kuendelea baada ya miaka.
Chanzo Cha Mwili Kuvimba
Ugonjwa hupelekea mwili kuvimba. Sasa swali laweza kuwa: Ni nini kinachosababisha mwili kuvimba? Mwili huvimba kwa sababu protini nyingi imepotea mwilini.
Kwa kawaida figo zina kichungi kinachochuja maji na uchafu kutoka kwenye damu hadi kwenye mkojo kinachoitwa glomeruli kama tulivyoona hapo juu. Kichungi hiki kina matundu madogo madogo sana yanayoruhusu kupita kwa vitu vidogo vidogo sana. Miongoni mwa vitu vinavyopita kwenye kichungi hiki ni pamoja na maji,chumvi,glucose na urea. Protein haiwezi kupita kwa sababu ni kubwa sana kuliko matundu yenyewe.
Mtu anapopata ugonjwa wa glomerulonephritis,matundu ya kichungi hiki hudhurika na kutanuka. Kitendo hiki husababisha na kuruhusu protein kupita na kuingia kwenye mkojo. Kwa sababu protein nyingi inapotea moja kwa moja kwa njia ya mkojo,damu hupungukiwa na protini. Damu inapokuwa na protin kidogo,husababisha mwili kuvimba.
Kiwango cha mwili kuvimba hutegemea kiasi cha protin iliyopotea. Protini nyingi ikipotea na kupungua mwilini,uvimbe wa mwili huwa mkubwa zaidi,na kama protini kidogo tu imepotea mwili huvimba kidogo tu.
Chanzo kikuu cha nephrotic syndrome ni ugonjwa wa glomerulonephritis.
Dalili Za Nephrotic Syndrome
Dalili zinazoonesha kuwa una ugonjwa unaosababisha mwili wako kuvimba ni kama zifuatazo:
-Mwili kujaaa maji hasa sehemu za miguu,mikono na kuzunguka macho yako
-Mkojo kuwa na protini nyingi
-Uzito kuongezeka kwa sababu ya ongezeko la maji
-Uchovu
-Kupoteza hamu ya kula
-Mafuta mengi kwenye damu
-Kiwango kidogo cha protini (albumin) kwenye damu
MadharaYa Ugonjwa Unaosababisha Mwili Kuvimba
Damu kuganda-hii ni kutokana na kupotea protini nyingi ambayo ingesaidia damu kuganda
Lehemu nyingi kwenye damu-kwa sababu ya kupungua protini,ini hutengeneza cholestrol nyingi na triglycerides
Kupungua uzito-kwa sababu ya kukosa hamu ya kula na ulaji dhaifu huweza kupelekea uzito kupungua
Shinikizo la juu la damu-kuharibika kwa vichujio vya figo (glomeruli),husababisha ongezeko kubwa la uchafu kwenye mishipa ya damu,na hivyo kupandisha shinikizo la damu.
Ugonjwa wa figo kushindwa ghafula-hii itatokana na uwezekano mkubwa wa uchafu kujikusanya kwenye figo kwa sababu ya kuharibika vichujio vya figo.
Ugonjwa sugu wa figo-hii ni kwa sababu uwezekano wa figo kuharibika kutokana na kurundikana kw auchafu
Maambukizi-watu wenye ugonjwa wa nephrotic syndrome huweza kuwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizi kwa urahisi.
Ndugu msomaji,kufikia hapo,tumefanikiwa kutazama kwa kina ugonjwa wa nephrotic syndrome-ambao husababisha mwili kuvimba. Huu nao ni ugonjwa mwingine wa figo unaochangia ugonjwa wa figo kushindwa kufanya kazi kabisa au ugonjwa wa figo kushindwa kufanya kazi ghafula.
Unahitaji kutunza afya ya figo zako? Tumia bidhaa tiba zinazoboresha afya ya figo zako ili kujiepusha na madhara zaidi ya figo zako. Kuagiza bidhaa za kutunza figo zako,bofya hapa-afya ya figo.
Wasiliana nasi kupitia afyagreen@gmail.com au unaweza kupiga +255 673 923 959.
Kwa maoni na ushauri,tuandikie kupitia afyagreen@gmail.com.