Ni ugonjwa unalofahamika kama Acute renal failure au Acute Kidney Failure. Ugonjwa wa figo wa muda hutokana na kupungua au kukoma kwa kazi ya figo kunakotokea ndani ya muda wa saa,siku au wiki kadhaa. Hali hii si ya kudumu na huweza kutibika au kurudia hali ya kawaida.
Figo kushindwa ghafula husababisha uchafu kujichanganya kwenye damu na kusababisha figo zishindwe kuweka msawazo wa maji maji vizuri mwilini. Ugonjwa wa figo wa muda mfupi huweza kuathiri viungo vingine kama vile ubongo,moyo na mapafu. Kushindwa ghafula kwa figo mara nyingi huwapata watu walio mahospitali,ICU na hususani kwa watu wenye umri mkubwa.
Dalili Za Ugonjwa Wa Figo Kushindwa Ghafula
Dalili za figo kushindwa ghafula huweza kuwa:
-Kupungua kiwango cha mkojo,japo wakati mwingine hubakia vile vile
-Miguu kujaa maji
-Kupumua kwa shida
-Uchovu (fatique)
-Kuchanganyikiwa
-Kichefuchefu
-Kuwa dhaifu (weakness)
-Mapigo ya moyo yasiyo sawasawa
-Maumivu ya kifua au presha
-Kuzimia
Chanzo Cha Figo Kushindwa Kufanya Kazi Ghafula
Figo kushindwa kufanya kazi kwa muda mfupi,huweza kusababishwa na mambo yafuatayo:
1. Kupungua kwa damu kwenye figo
2. Figo kudhurika moja kwa moja
3. Mkojo kuzuiwa kutoka nje ya mwili
Hebu tuzitazame sababu hizi kwa kina sasa:
1. Kupungua damu kwenye figo
Magonjwa an matatizo yanayoweza kusababisha damu kupungua kwenye figo na kusababisha kushindwa ghafula kwa figo ni kama yafuatayo:
-Kupoteza damu au maji mwilini kwa njia ya kutoka damu,kuhara n.k
-Dawa za kupunguza shinikizo la juu la damu au kuwa na shinikizo la chini la damu
-Shambulio la moyo (heart attack),kushindwa kwa moyo (heart failure) na mengineyo yawezayo kupunguza utendaji kazi wa moyo
-Maambukizi
-Ini kushindwa
-Kutumia zaidi dawa za maumivu (NSAIDs- Non-Steroidal Anti-inflammatory Drugs) ambazo hutumika kuondoa uvimbe,maumivu yatokanayo na kichwa kuuma,baridi,mafua na mengineyo. Madawa hayo ni kama vile asprin,ibuprofen,ketoprofen na naproxen
-Kuwa na mzio (allergy)
-Kuungua
-Upasuaji mkubwa
-Ajali
2. Figo kudhurika moja kwa moja
Kuna baadhi ya magonjwa na matatizo huweza kusababisha figo zako kushindwa kufanya kazi kwa muda mfupi. Matatizo na magonjwa hayo ni kama yafuatayo:
-Damu kuganda kwenye mishipa ya ateri na vein za figo au zinazozunguka figo zako
-Kugandamana kwa lehemu (cholesterol) kwenye figo kunakozuia mtiririko wa damu kwenye figo
-Glomerulonephritis
-Hemolytic Uremic Syndrome
-Maambukizi
-Madawa kama vile dawa fulani za chemo,antibiotic na dyes ambazo hutumika wakati wa vipimo vya picha
-Scleroderma- ugonjwa unaoathri ngozi na tishu zake
-Sumu kama vile pombe,metali nzito na cocaine
-Kuvunjwa kwa tishu za misuli kunakozalisha sumu inayoharibu figo
-Kuvunjwa kwa seli za uvimbe kunakozalisha sumu inayoharibu figo
3. Mkojo kuzuiwa ndani ya figo
Yapo magonjwa na hali fulani za kiafya zinazoweza kusababisha mkojo ukazuiwa ndani ya figo na usitolewe nje. Magonjwa na hali hizo ni kama:
-Kansa ya mfuko wa mkojo
-Damu kuganda kwenye njia ya mkojo
-Kansa ya shingo ya kizazi
-Kansa ya utumbo mpana
-Tezi dume iliyovimba
-Mawe kwenye figo
-Kuharibika neva zinazoratibu kibofu cha mkojo
-Kansa ya tezi dume
Sababu Hatarishi Za Ugonjwa Wa Figo Kushindwa Ghafula
Kuna baadhi ya mambo au magonjwa ambayo huhatarisha mtu kupata tatizo la figo kushindwa kufanya kazi kwa muda mfupi. Hizi ni baadhi ya sababu hatarishi zinazoweza kukufanya ukapatwa na ugonjwa wa figo kushindwa ghafula kutenda kazi zake. Sababu hizo ni kama:
-Kulazwa hospitali kutokana na tatizo linalohitaji uangalizi makini
-Kuwa na umri mkubwa
-Kuziba kwa mishipa ya damu miguuni na mikononi
-Kisukari
-Tatizo la shinikizo la juu la damu
-Moyo kushindwa (heart failure)
-Magonjwa ya figo
-Magonjwa ya ini
-Aina fulani za kansa na tiba zake
Hatari/Madhara Ya Figo Kushindwa Kufanya Kazi Ghafula
Maji kwenye mapafu- figo zikishindwa kufanya kazi kwa ghafula,husababisha maji kuongezeka kwenye mapafu na kusababisha kupumua kwa shida
Maumivu kifuani-maumivu haya hutokea pale kuta zinazozunguka moyo zinapokuwa zimedhurika.
Misuli dhaifu-hutokea pale kunapokosekana uwiano kati ya maji maji na vitu vigumu (madini na chumvi) mwilini.
Kudhurika kwa kudumu kwa figo-tatizo la kudhurika kwa muda huweza kusababisha figo kupata athari ya kudumu.
Kifo-figo kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa huweza kusababisha mgonjwa kufariki.
Matibabu Ya Ugonjwa Wa Figo Wa Muda
Mambo haya yakifanyika huweza kusaidia kama tiba ya ugonjwa wa figo kufeli kwa muda:
1. Kutibu chanzo cha ugonjwa wa figo
Ili kutibu tatizo hili ni muhimu sana kubaini chanzo cha tatizo hili. Matibabu sahihi ya chanzo kama vile shinikizo la damu,maambukizi,kuziba mirija ya mkojo n.k huweza kuponya figo.
2.Kutumia dawa
Mgonjwa atatumia dawa kulingana na chanzo husika cha tatizo lake.
3.Matumizi ya chakula
Lishe bora ni muhimu sana kwa mgonjwa mwenye ugonjwa wa figo kufeli. Mgonjwa anashauriwa kutumia matunda na juisi za matunda kwa wingi huku akiepuka kutumia chumvi kwa wingi kwa sababu itachangia kuongeza tatizo.
4.Dayalisisi
Hii ni njia mbadala ya ufanyaji kazi wa figo kwa kutumia mashine. Hii huwasaidia watu wale ambao figo zao zimefeli kabisa. Mgonjwa wa ugonjwa wa figo kufeli kwa muda huhitaji dayalisisi kama kuna dalili endelevu za figo kufeli.
Naam ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala hizi za afya,hapa tumetazama kwa kina tatizo la figo kufeli kwa ghafula. Tutaendelea kuyatazama matatizo na magonjwa mengine ya figo katika makala zetu zinazokuja. Mada itakayofuata tutazama Ugonjwa Wa Kudumu Wa Figo Kushindwa. Tafadhali endelea kufuatana nasi.
Ndugu msomaji wangu huenda unasumbuliwa na ugonjwa wa figo na unatafuta kwa karibu kupata tiba. Kama umefanikiwa kupata tiba au ndo unatafuta tiba sasa,wasiliana nasi kupata bidhaa tiba kwa ajili ya afya ya figo. Dawa hizi zitasaidia kusafisha figo,kuzipa figo uwezo wa utendaji wake na kuepusha madhara zaidi ya ugonjwa wowote wa figo.
Tafadhali wasiliana nasi kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.