TATIZO LA KUKOSA CHOO

Unaweza kulichukulia kuwa tatizo la kawaida lakini likidumu kwa muda mrefu,kuwa na choo kigumu au kufunga choo kabisa kunaweza kuku... thumbnail 1 summary







Unaweza kulichukulia kuwa tatizo la kawaida lakini likidumu kwa muda mrefu,kuwa na choo kigumu au kufunga choo kabisa kunaweza kukusababishia matatizo makubwa. Lakini kwanza hebu tutazame inavyowea kutokea ukakosa choo au ukawa na choo kigumu.



Chanzo Cha Kukosa Choo




1.Kukosa chakula cha nyuzi nyuzi-hiki huboresha mtiririko wa chakula tumboni na kulainisha choo. Vyakula vya nyuzi nyuzi kwa wingi ni kama matunda,mbogamboga pamoja na nafaka nzima.

2.Kukosa mazoezi,kwa sababu mzoezi haharakisha uvunjwaji wa chakula ili kutengeneza nishati,na hivyo kufanya mzunguko wa chakula tumboni kuwa mzuri.

3.Kutumia madawa kwa wingi-baadhi ya madawa huweza kukausha maji na kusababisha choo kuwa kigumu

4.Maziwa-baadhi ya watu hukosa choo kwa sababu ya maziwa

5.Wajawazito-kwa sababu ya mabadiliko ya homoni wajawazito huweza kukosa choo. Lakini pia mfuko wa mimba huweza kugandamiza tumbo na kupunguza mwendo wa chakula

6.Umri-kwa kadri umri unavyoongezeka,kasi ya kuvunja chakula na kutengeneza nishati hupungua pia na kusababisha chakula kujivuta

7. Kubadilisha mazingira-unapotoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine au unapobadilisha ratiba iliyokuwa imezoelea mwilini,kula au kulala muda tofauti, huweza kupelekea kufunga choo kwa muda

8.Kutokwenda chooni kwa wakati-kuna watu hupuuzia kwenda chooni pale wanapohisi haja. Hii husababisha choo kuzidi kuwa kigumu kusababisha ugumu wa kujisaidia.



9.Kushindwa kunywa maji ya kutosha-hii hupelekea choo chako kuwa kigumu,hata hivyo kunywa maji mara kwa mara huweza kuondoa hatari ya kufunga choo

10. Kutumia caffeine-vinywaji vyenye caffeine huwa na tabia ya kufyonza maji na kukausha mwili



Madhara Ya Kufunga Choo



Japo siyo tatizo hatarishi sana,lakini ukikosa choo kwa muda mrefu huweza kusababisha madhara kama:

1. Kuchanika sehemu ya kutolea haja kubwa

2. Kutoa kinyesi chenye damu

3.Bawasiri-kuvimba kwa mirija ya vein inayozunguka sehemu ya kutolea haja kubwa


Jinsi Kuondoa Tatizo La Kufunga Choo

Kufanya choo chako kiwe laini na kuepukana na kupata choo kigumu na kufunga choo,fanya yafuatayo:

-Kunywa maji ya kutosha

-Kula vyakula vya nyuzi nyuzi kwa wingi

-Epuka kutumia vinywaji vyenye caffeine

-Fanya mazoezi mara kwa mara

-Epuka kuzuia choo pale unapojisikia kwenda kujisaidia

-Tumia dawa kama limekuwa tatizo endelevu


Ndugu msomaji wangu,kwa ufupi kabisa tulikuwa tunatazama tatizo la kukosa choo. Inawezekana unahitaji kupata ahueni kutokana na tatizo hili kwa haraka kutokana na jinsi linavyokusumbua. Unaweza kutumia bidhaa hizi zisizo na kemikali ili kuweka mtiririko wako wa chakula sawasawa.

Kupata dawa ya kuondoa kufunga choo,bofya hapa: Dawa ya kukosa choo

Kwa ushauri,maoni,swali na mengineyo,tafadhali tuandikie kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.