UGONJWA WA MAFUTA KWENYE INI-FATTY LIVER DISEASE

Mwili hutunza mafuta sehemu mbali mbali za mwili kwa ajili ya kutengeneza nishati na kuunda ngozi. Ini pia limeundwa na kiwango fula... thumbnail 1 summary




Mwili hutunza mafuta sehemu mbali mbali za mwili kwa ajili ya kutengeneza nishati na kuunda ngozi. Ini pia limeundwa na kiwango fulani cha mafuta yatakiwayo kutumiwa mwilini. Endapo kiwango cha mafuta kwenye ini kitaongezeka sana,huonesha kwamba hilo ni tatizo la kiafya.

Ugonjwa wa ini kuwa na mafuta mengi humweka mtu katika hatari ya kupata magonjwa mbali mbali kwa sababu huharibu ini kwa haraka. Kwa kawaida ini hufanya kazi nyingi sana mwilini zikiwemo kuondoa sumu mwilini na kutengeneza nyongo inayomeng'enya mafuta mwilini. Sasa ini likiharibika kazi hizi zote hushindwa kufanyika na kusababisha madhara ya kutosha mwilini.



Aina Za Ugonjwa Wa Ini Lenye Mafuta


Kuna aina mbili za msingi za ugonjwa wa ini lenye mafuta. Aina hizo ni:

1. Nonalcoholic Fatty Liver Disease (NAFLD)

Ugonjwa huu hutokea pale ini linaposhindwa kuvunja vunja mafuta kwenye ini na kusababisha mafuta kujijenga kwenye tishu za ini. Chanzo cha ugonjwa huu hakihusiani na pombe,na huweza kugunduliwa pale mafuta yanapofikia zaidi ya asilimia 5 ya ini.

Chini ya aina hii ya ugonjwa wa ini lenye mafuta,kuna:

 -Nonalicoholic Steatohepatitis (NASH)

Ni aina ya NAFLD. Mafuta yanapojijenga kwenye kuta za ini husababisha maambukizi. Asilimia 5 ya ini inapokuwa ni mafuta,na maambukizi yakawepo kwenye ini,hali hiyo ndiyo huwa NASH.

Dalili zake huweza kuwa: kupoteza hamu ya chakula,kichefuchefu,kutapika,njano na maumivu ya tumbo. Kama litaachwa bila kutibiwa,steatohepatitis huweza kusababisha makovu kwenye ini,kansa ya ini na hatimaye hupelekea ini kufeli.


-Acute fatty liver of pregnancy

Hutokea kwa nadra sana lakini ni tatizo hatarishi kwa wajawazito.

Dalili zake huanza kuonekana katika miezi mitatu ya mwisho. Dalili hizo huweza kuwa: kichefuchefu na kutapika kwingi,maumivu upande wa juu wa tumbo kulia,kichwa kuuma,njano,kupoteza hamu ya kula na uchovu.

2. Alicoholic Fatty Liver

Unywaji pombe kupita kiasi huharibu ini na matokeo yake hushindwa kuvunja mafuta. Kuacha kunywa pombe husaidia ini lenye mafuta angalau kuimarika. Ndani ya wiki 6 za kutokunywa pombe,mafuta huweza kupotea. Lunywaji pombe utaendelea kwa kiwango cha juu,huweza kusababisha maambukizi yanayopelekea ini kuharibika kabisa.



Chanzo Cha Ugonjwa Wa Ini Lenye Mafuta



Sababu kubwa ni unywaji pombe. Lakini pia mbali na pombe sababu zingine ni:

-Unene kupita kiasi

-Kiwango kikubwa cha mafuta kwenye damu

-Kisukari

-Magonjwa ya vinasaba-magonjwa ya kurithi

-Kupungua uzito ghafla

-Madhara yatokanayo na magonjwa kama methotrexate,tamoxifen,amiodorone n.k

-Shinikizo la damu

-Kuwa na saizi kubwa ya kiuno

-Kuwa na sukari nyingi kwenye damu



Sababu Hatarishi Za Ini Kuwa Na Mafuta



Ini lako laweza kujaa mafuta,endapo:

-Unakunywa pombe kwa wingi

-Unakunywa dawa bila kufuata maelekezo

-Ni mjamzito

-Una lehemu nyingi

-Kiwango cha triglyceride kiko juu

-Una Utapiamlo

-Mwili dhaifu usio na mazoezi



Jinsi Ya Kujikinga Na Ini Tatizo Ini Kuwa Na Mafuta



-Punguza au acha kunywa pombe

-Kula mlo kamili

-Dhibiti kisukari 

-Fanya mazoezi kila siku angalau dakika 30 kwa siku.


Mada itakayofuata tutaangalia ugonjwa mwingine wa ini. Usiende mbali,endelea kuwa nasi.
Fanya kila linalowezekana kutunza ini lako. Wasiliana nasi kupata dawa za kuondoa mafuta kwenye ini lako. Wasiliana nasi kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959 sasa.

Usisahau kuacha maoni,ushauri au swali lako kunako afyagree@gmail.com.