Maambukizi kwenye figo ni moja ya magonjwa yatokanayo na maambukizi katika njia ya mkojo. Maambukizi haya huanzia kwenye mirija ya urethra au kwenye kibofu na kuenea hadi kwenye figo. Inaweza kuathirika figo moja au figo zote kuathirika.
Maambukizi kwenye figo huhitaji uangalizi wa mapema. Kama tatizo hili halitatibiwa mapema figo huweza kuharibika kabisa. Lakini pia bakteria huweza kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na kusababisha maambukizi yanayohatarisha maisha.
Dalili Za Maambukizi Kwenye Figo
Dalili za maambukizi kwenye figo ni kama zifuatazo:
-Homa
-Baridi na kutetemeka
-Maumivu mgongo,tumbo chini ya mbavu na nyonga
-Maumivu ya tumbo
-Kukojoa mara kwa mara
-Hamu ya kukojoa isiyoisha
-Maumivu yanayochoma wakati unakojoa
-Kichefuchefu na kutapika
-Kukojoa mkojo wenye damu
-Kukojoa mkojo unaonuka sana au mweusi
Chanzo Cha Kupata Maambukizi Kwenye Figo
Chanzo cha maambukizi kwenye figo ni maambukizi kwenye mirija ya urethra na kibofu cha mkojo. Bakteria wanaosababisha maambukizi kwenye mirija ya urethra na kwenye kibofu cha mkojo husafiri na kuingia kwenye figo. Na hapo husababisha maambukizi kwenye figo.
Wakati mwingine maambukizi mahali kwingineko mwilini huweza kusafirishwa na kupitia mishipa ya damu hadi kwenye figo. Japo si rahisi kusababisha maambukizi kwenye figo,huweza kutokea kama una joint bandia au kama una maambukizi kwenye chemba za moyo.
Mara chache sana maambukizi kwenye figo huweza kusababishw ana upasuaji wa figo.
Sababu Hatarishi Za Kupata Maambukizi Kwenye Figo
Unaweza kuwa kwenye hatari ya kupata maambukizi ya figo kama:
Ni mwanamke-kwa wanawake mirija ya urethra ni mifupi sana kiasi cha bakteria kusafiri haraka kufikia kibofu cha mkojo. Lakini pia ni karibu na sehemu ya haja kubwa,jambo linaloongeza uwezekano mwingine wa kupata maambukizi ya bakteria kwa urahisi.
Akina mama wajawazito wana hatari kubwa zaidi ya kupata maambukizi haya ya figo.
Njia ya mkojo imeziba-kukiwa na kizuizi chochote kwenye njia ya mkojo kinachozuia mkojo kutoka kwa urahisi, kama vile,mawe kwenye figo au kuvimba tezi dume kwa wanaume,huongeza uwezekano wa kupata maambukizi kwenye figo
Mfumo wa kinga ni dhaifu-hii hutokana na kuwa na kuwa na matatizo au magonjwa yanayodhoofisha mfumo wa kinga kama vile Ugonjwa wa kisukari na VVU.
Neva zinazozunguka kibofu cha mkojo zimeharibika-hupumbaza mwili usigundue maambukizi kwenye kibofu na hatimaye hufikia figo
Unatumia mpira wa mkojo-kutokana na upasuaji au ugonjwa wowote unaokuweka kitandani. Kupatwa na maambukizi inakuwa rahisi sana.
Madhara Ya Maambukizi Kwenye Figo
Madhara ya maambukizi sugu kwenye figo ni haya:
Makovu kwenye figo-hupelekea magonjw aya figo kama shinikizo la damu na figo kushindwa kabisa.
Sumu kwenye damu-kwa vile figo huchuja uchafu kutoka kwenye damu,na kama figo zina maambukizi,maambukizi yaweza kuenea hadi kwenye mishipa ya damu
Matatizo kwa mama mjamzito-anaweza kujifungua mtoto mwenye uzito kidogo au njiti kutokana na maambukizi kwenye figo.
Jinsi Ya Kuepuka Na Maambukizi Kwenye Figo
-Kunywa maji kwa wingi
-Kojoa kila unapohisi kubanwa
-Kojoa kila baada ya kufanya tendo la ndoa
-Jisafishe kwa umakini-kutokea mbele kwenda nyuma
-Usitumie manukato na marashi kwenye nyeti zako
Ni ugonjwa mwingine wa figo-maambukizi kwenye figo. Tumeweza kutazama vyema maambukizi kwenye njia ya mkojo-Ugonjwa wa UTI,Ugonjwa wa kisukari wa figo na magonjwa mengine ya figo. Nadhani ni wakati mwafaka kwako kupata dawa bora za kutunza figo zako,kwa sababu tumegundua ni muhimu,kabla hujafikia figo kuharibika kabisa. Ungana nasi katika mada inayofuata kulitazama ugonjwa wa figo kujaa maji.
Unaweza kupata tiba na dawa ya kurejesha ubora wa utendaji kazi wa figo ili kuepuka madhara ya figo zaidi. Wasiliana nasi kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.