UGONJWA WA KISUKARI WA FIGO-DIABETIC NEPHROPATHY

Huu ni ugonjwa mwingine wa figo. Ni ugonjwa wa figo kwa mgonjwa mwenye tatizo la kisukari. Inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya watu wenye u... thumbnail 1 summary



Huu ni ugonjwa mwingine wa figo. Ni ugonjwa wa figo kwa mgonjwa mwenye tatizo la kisukari. Inakadiriwa kuwa asilimia 40 ya watu wenye ugonjwa wa kisukari hupata ugonjwa huu wa figo. Ni ugonjwa hatari sana unaowapata wagonjwa wenye kisukari aina ya 1 na 2.

Aina hii ya ugonjwa wa figo huathiri uwezo wa figo kufanya kazi yake ya kuondoa uchafu na maji yaliyozidi mwilini. Njia pekee ya kuepuka au kuzuia ugonjwa wa kisukari wa figo,ni kudumisha mfumo bora wa maisha,kutibu ugonjwa wa kisukari na kutibu ugonjwa wa shinikizo la damu.


Ugonjwa wa kisukari wa figo huongezeka taratibu mwaka baada ya mwaka,na kama hautatibiwa mapema,husababisha ugonjwa sugu wa figo,ambao ni hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo isiyokuwa na tiba. Katika hatua hii mgonjwa hutakiwa kufanyiwa dayalisisi au kubadilishiwa figo ili aweze kuishi.

Tiba ya mapema kwa mgonjwa wa figo,huweza kupunguza makali ya ugonjwa na kuzuia madhara zaidi.



Dalili Za Mgonjwa Wa Kisukari Na Figo



Katika hatua za mwanzo,unaweza usione wala kuhisi dalili zozote. Ila katika hatua za badaye,unaweza kuona dalili zifuatazo:

-Kushindwa kudhibiti shinikizo la damu

-Kukojoa mkojo wenye protini

-Kuvimba miguu,mikono na macho

-Kuwa na hamu ya kukojoa mara kwa mara

-Kuchanganyikiwa au kupoteza utulivu

-Kupoteza hamu ya kula

-Kutohitajika kwa insulini au madawa ya kisukari

-Kichefuchefu na kutapika

-Miwasho isiyoisha

-Uchovu


Chanzo Cha Ugonjwa Wa Kisukari Wa Figo



Ugonjwa wa kisukari wa figo hutokea pale sukari (diabetes) inapoharibu mishipa ya damu na seli zingine ndani ya figo. Hutokea kwa wagonjwa wenye kisukari aina zote za kisukari yaani aina ya 1 na 2. Ugonjwa wa kisukari usipotibiwa kwa muda mrefu,husababisha mgandamizo mkubwa kwenye vichujio vya figo (glomeruli) na hivyo kuharibu figo kabisa.


Sababu Hatarishi Za Ugonjwa Wa Kisukari Wa Figo:



Unaweza kupata ugonjwa huu kama:

-Una kisukari aina ya 1 au 2

-Una sukari nyingi kwenye damu (hyperglycemia) ambayo huwezi kuidhibiti

-Una shinikizo la damu (hypertension) na huwezi kulimudu

-Unavuta sigara na una ugonjwa wa kisukari

-Una lehemu nyingi na una ugonjwa wa kisukari

-Ni mwanafamilia yenye historia ya magonjw aya kisukari na figo



Madhara Ya Ugonjwa Wa Kisukari Wa Figo




Madhara ya ugonjwa huu huanza na kuendelea taratibu baada ya miezi au miaka kadhaa,nayo huweza kuwa:

-Mwili kujaaa maji yanayopelekea miguu na mikono kuvimba,shinikizo la damu,mapafu kujaa maji (pulmonary edema)

-Kuongezeka kiwango cha potasium kwa ghafula (hyperkalemia)

-Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu yanayoweza kupelekea kiharusi

-Mishipa ya damu ndani ya retina kuharibika

-Upungufu wa damu (Anemia)

-Matatizo ya kuharibika mishipa ya damu na neva kama vile vidonda miguuni,jogoo kushindwa kusimama,kuharisha n.k

-Madhara kwa mjamzito hadi kwa mtoto tumboni

-Ugonjwa wa kudumu wa figo



Kujikinga Na Ugonjwa Wa Kisukari Wa Figo




Ili kujikinga na ugonjwa huu hatari:

Tibu ugonjwa wa kisukari-kama utapata tiba ya kisukari mapema,unaweza kuepuka au kupunguza ukali na madhara ya ugonjwa wa kisukari wa figo

Tibu shinikizo la damu na magonjwa mengine yanayoharibu figo-kama una tatizo la shinikizo la juu la damu au magonjwa mengine yanayopelekea kupata ugonjwa wowote wa figo,tafuta tiba mapemma ili kuepuka madhara zaidi

Tumia dawa kwa uangalifu-tumia dawa za kupunguza maumivu (NSAIDs) kwa uangalifu. Kwa wagonjwa wa kisukari matumizi ya dawa za kupunguza maumivu huweza kuharibu figo zako

Kuwa na uzito unaofaa-anza mpango wa kupunguza uzito wako,ongea na daktari wako kuhusu mazoezi unayotakiwa kufanya na chakula unachotakiwa kutumia ili kuwa na uzito unaofaa.

Usivute sigara-uvutaji wa sigara huharibu figo zako mara moja. Pata ushauri wa kitalamu kwa daktari na washauri wa afya jinsi ya kuacha sigara.

Unaweza kuanza tiba ya ugonjwa wa kisukari wa figo sasa. Kuanza tiba ya ugonjwa wa kisukari wa figo,bofya hapa chini. Kuweka oda yako bofya weka order sasa. Tuandikie kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.

Ndugu msomaji tumefanikiwa kutazama ugonjwa mwingine wa figo-ugonjwa wa kisukari wa figo katika mada hii. Mada zilizopita tulitazama ugonjwa wa kuharibika vichujio vya figo na ugonjwa wa figo unaosababisha mwili kuvimba.  Mada zitazofuata tutajadili magonjwa mengine ya figo-ugonjwa wa UTI,maambukizi kwenye figo na mengineyo.

Kwa maoni,ushauri na maswali,tyuandikie kupitia afyagreen@gmail.com.