DEEP SEA FISH OIL SOFTGEL

Kazi Na Faida Zake .Hupunguza kiwango cha lipids (fats,cholestrol na triglycerides) ndani ya damu .Hupunguza uvimbe ndani ya mwili ... thumbnail 1 summary




Kazi Na Faida Zake


.Hupunguza kiwango cha lipids (fats,cholestrol na triglycerides) ndani ya damu
.Hupunguza uvimbe ndani ya mwili
.Hupunguza kujikusanya kwa platelets;huzuia kuganda kwa damu kwa wingi
.Huzuia kutanuka kwa mishipa ya arteri;hutanua arteri n akuzipa utulivu


Hufaa Kwa:


.Watu wenye matatizo ya ubongo na moyo
.Watu wenye sukari 2
.Watu wenye matatizo ya mifupa na maungio ya mifupa kama vile osteoporosis na Arthritis
.Watu wazima walio na upungufu wa kula omega-3 fatty acids


Viungo: Deep sea fish oil extract,EPA:180mg/capsule;DHA:120mg/capsule



Maelezo Muhimu




Omega-3 fatty acids


Virutubisho vitatu muhimu vya omega-3 fatty acids ni alpha-linolenic acid,eicosapentaenoic acid (EPA) na docosahexaenoic acid (DHA). Mwili hubadili alpha-linoleic kuwa EPA na DHA,ambazo pia huweza kupatikana moja kw amoja toka kwenye baadhi ya mimea,mara nyingi samaki wa maji baridi kama vile salmon,tuna,halibut na herring. EPA hufanya kazi kubwa ya kuzuia magonjwa ya moyo wakati DHA ni muhimu kwa ajili ya utendaji kazi bora wa ubongo na maendeleo ya neva.


Kwa Ajili Ya Afya Kuta Za Seli (cell membrane)


Seli isiyo na membrane yenye afya hupoteza uwezo wa kutunza maji na na virutubisho muhimu. Lakini pia hupoteza uwezo wa kuwasiliana na seli zingine. Watafita wanaamini kuwa kupoteza mawasiliano kati ya seli na seli,huweza kupelekea kukua kwa seli za kansa.

Kwa sababu kuta za seli (cell membranes) zimetengenezwa na mafuta utendaji kazi na uwingi wa maji kwenye kuta hizi hutambuliwa na aina ya mafuta tunayokula. Kumbuka kuwa mafuta ya kawaida katika jotoridi la kawaida huwa ni yabisi wakati omega-3 fatty acid katika jotoridi la kawaida huwa ni kimiminika. Watafiti wanaamini kuwa chakula cha mafuta ya kawaida kwa wingi hutengeneza kuta yabisi na zisizo na maji wakati ulaji wa omega-3 fatty acid hutengeneza kuta za seli zenye maji maji kwa wingi.


Uwezo Wa Kuondoa Uvimbe


Ugunduzi wa hivi karibuni kuwa miili yetu hutengeneza Resolvins kutokana na EPA husaidia kuelezea kwa nini omega-3 fatty acids huweza kuondoa uvimbe kwenye maungio ya mifupa yetu na kuboresha mtiririko wa damu.

Resolvins hutengenezwa kutokana na EPA na enzyme zilizo ndani ya seli na hufanya kazi kwa kuzuia na kudhibiti uhamiaji wa seli za uvimbe na kemikali kwenye eneo la uvimbe. Tofauti na madawa ya kuzuia uvimbe kama vile asprins,ibuprofen na COX-2 inhibitors,resolvin hii inayotengenezwa na miili yetu, haina madhara ndani ya tumbo na kwenye mishipa ya moyo.


Manufaa Kwenye Ubongo Na Moyo


EPA husaidia kuondoa hatari ya kupata magonjwa ya moyo kama vile cholestrol na high blood pressure. Deep Sea Fish Oil imebainika kuwa na uwezo wa kupunguza kiwango cha triglycerides na hivyo kupunguza hatari ya kifo,shambulio la moyo,kiharusi,na matatizo ya moyo kwa yeyote aliyewahi kuwa na shambulio la moyo. Deep Sea Fish Oil pia huzuia na kutibu tatizo la atherosclerosis kwa kupunguza utengenezwaji wa plaque na damu kuganda vinvyoweza kuziba arteri.


Manufaa Yake Kwa Wagonjwa Wa Kisukari


Watu wenye kisukari kwa kawaida huwa na kiwango kikubwa cha triglycerides na kiwango kidogo cha HDL. Omega-3 fatty acid inayotokana na Deep Sea Fish Oil husaidia kupunguza triglycerides na apoprotein (ambazo husababisha kisukari), na kuongeza kiwango cha LDL. Aina nyingine ya omega-3 fatty acid,ALA (inayookana na flaxseed kwa mfano) haziwezi kuwa na manufaa kama ya Deep Sea Fish oil. Watu wengine wenye kisukari hawawezi kwa ufasaha kubadili ANA kuwa EPA na DHA. Kupata omega-3 fatty acid kutoka kwenye Deep Sea Fish Oil ni muhimu sana kwa watu wenye kisukari 2.

Nunua Deep Sea Fish Oil sasa: