UGONJWA WA FIGO WA POLISTIKI-POLYCYSTIC KIDNEY DISEASE (PKD)

Ni ugonjwa wa figo wa kurithi unaotokana na hitilafu kwenye vinasaba. Ugonjwa huu husababisha uvimbe kutokea ndani ya figo. Vibofu hiv... thumbnail 1 summary




Ni ugonjwa wa figo wa kurithi unaotokana na hitilafu kwenye vinasaba. Ugonjwa huu husababisha uvimbe kutokea ndani ya figo. Vibofu hivi vya uvimbe ndani ya figo husababisha figo kuvimba na kuongezeka ukubwa kuliko kawaida. Hali hii huharibu tishu za figo na kusababisha ugonjwa sugu wa figo unaopelekea figo kushindwa kufanya kazi kabisa.

Ugonjwa wa figo wa uvimbe uliojaa maji husababishwa na hitilafu katika vinasaba. Ugonjwa huu hurithiwa toka kwa wazazi hadi kwa watoto.

Bado hakuna tiba,ila unaweza kupunguza hatari zitokanazo na ugonjwa huu wa figo kwa kupunguza dalili za ugonjwa huu.


Chanzo Na Aina  Za Ugonjwa wa figo wa uvimbe uliojaa maji


Ziko aina mbili za ugonjwa wa polistiki. Aina hizi hutokana na visababishi vyake:

1. Autosomal Dominant Polycystic Kidney Disease (ADPKD)

Ni aina ya ugonjwa wa figo wa polistiki ambao husababisha vibofu vya uvimbe (cysts) kwenye figo pekee. Mara nyingi huitwa ugonjwa wa watu wazima (Adult Polycystic kidney disease) kwa sababu dalili zake huonekana mtu anapokuwa na umri kati ya miaka 30 na 50. Mtu hupata ugonjwa huu kama mzazi mmoja ana vinasaba vya ugonjwa huu. Asilimia 90 ya wagonjwa wa polistiki huwa na aina hii ya kwanza.

2. Autosomal Recessive Polycystic Disease (ARPD)

Aina hii ya ugonjwa wa figo wa polistiki husababisha vibofu vya uvimbe (cysts) kwenye figo na ini. Kwa aina hii ya ugonjwa wa figo wa uvimbe unaotoa maji huonesha dalili huonekana katika umri mdogo sana wa miezi,siku au hata kabla ya mtoto kuzaliwa.

Wazazi wote wawili hutakiwa kuwa na aina hii ya ugonjwa ndipo utarithiwa na mtoto. Kama mzazi mmoja tu ndiye mwenye ugonjwa huu,hautaweza kurithiwa.


Dalili Za Ugonjwa Wa Figo Wa Uvimbe Unaotoa Maji



-Shinikizo la damu

-Maumivu ya mgogo (upande mmoja au pande zote),mbavu au tumbo kuvimba

-Kuhisi uvimbe wa tumbo

-Damu au protini kwenye mkojo

-Maambukizi ya njia ya mkojo mara kwa mara

-Mawe kwenye figo

-Ugonjwa sugu wa figo

-Maambukizi kwenye figo

-Kuvimba tumbo kutokana na kuvimba figo

-Kichwa kuuma

-Kukojoa mara kwa mara


Madhara Ya Ugonjwa Wa Figo Wa Polistiki


Shinikizo la damu-kutotibu shinikizo la damu mapema huweza kuongeza madhara zaidi ikiwemo figo kufeli kabisa.

Figo kupoteza ubora wake-figo huendelea kuharibika taratibu na kupoteza ubora wake

Matatizo kwa mama mjamzito-akina mama wanaweza kupata ujauzito hata kama wana ugonjwa wa figo wa polistiki,lakini huleta hatari wakati wa kujifungua kama preeclampsia-shinikizo la damu,mwili kujaa maji na mkojo wenye protini kwa wingi.

Ini kujaa maji-vibofu vya maji vikijaa kwenye ini,husababisha ini kujaa. Ni tatizo linalotokea zaidi kwa wanawake kwa sababu homoni za kike huchangia.

Uvimbe kwenye ubongo-watu wenye ugojwa wa figo kujaa maji,huhatarisha kupata uvimbe kwenye ubongo.

Matatizo ya utumbo mpana-utumbo kuwa dhaifu sana na kuvimba

Maumivu yasiyoisha-hutokea maeneo ya mgongo na pembezoni. Huweza pia kuhusianishwa pia na maambukizi kwenye njia ya mkojo na mawe kwenye figo.


Madhara mengine ni kama yafuatayo:



-Uvimbe wa maji maji kwenye kongosho na korodani

-Kushindwa kuona vizuri na upofu

-Magonjwa ya ini

-Upungufu wa damu/anemia

-Ini kufeli

-Magonjwa ya moyo

-Kutokwa damu au kupasuka kwa vibofu vya maji


Jinsi Ya Kujiepusha Na Ugonjwa Wa Figo Wa Polistiki



Pamoja na kufanya kila linalowezekana kuimarisha afya ya figo zako,fanya mambo yafuatayo:

Tibu ugonjwa wa shinikizo la damu

-Kula vyakula visivyokobolewa (nafaka nzima),matunda,mboga za majani kwa wingi na chumvi kidogo sana.

-Punguza uzito wako

-Acha kuvuta sigara

-Fanya mazoezi mara kwa mara angalau dakika 30 kila siku

-Acha kunywa pombe


Tumetazama kwa kina ugonjwa wa figo-uvimbe unaotoa maji. Naamini umenufaika na mada za kutosha kuhusiana na magonjwa ya figo,na umeelewa unaumwa ugonjwa gani wewe. Ni muhimu kujiepusha na madhara mengi ya magonjwa haya kwa sababu ni hatari sana.

Unaweza kuwasiliana nasi kupata bidhaa tiba bora-kwa afya ya figo,ili kudhibiti magonjwa ya figo na kuepuka madhara zaidi. Tuandikie kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie kupitia +255 673 923 959.


Kwa maoni,ushauri na maswali,unaweza kutuandikia kupitia afyagreen@gmail.com.