Kabla ya kulifahamu tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo,hebu kwanza fahamu kwa ufupi nyongo ni nini na kazi yake ni ipi. Si hivyo tu bali pia nataka ufahamu mfuko wa nyongo ni nini na una kazi gani ndipo ufahamu jinsi mawe yanavyotokea kwenye mfuko wa nyongo.
Nyongo ( Bile) Ni Nini?
Nyongo ni juisi inayotumika kumeng'enyea chakula ambayo huzalishwa na ini na kutunzwa ndani ya mfuko wa nyongo. Nyongo haina kimeng'enya (enzymes) lakini ina asidi inayosaidia kumeng'enya mchanganyiko wa mafuta mwilini.
Kazi Za Nyongo
Nyongo ina kazi kubwa mbili:
Kusaidia umeng'enywaji wa mafuta na kusharabiwa kwenye utumbo mwembamba-Chumvi chumvi iliyo kwenye nyongo hujishikiza na mafuta yanayotokana na chakula na kupenya kuingia kwenye mishipa ya damu na badaye hurejeshwa kwenye nyongo.
Kusaidia kutoa uchafu nje toka kwenye damu- Mwili una kawaida ya kuvunja chembe hai nyekundu za damu zilizozeeka na kutengeneza mpya. Nyongo ndio huchua mabaki haya (bilirubin) na kutoa ncje kama uchafu.
Mfuko Wa Nyongo (Gallbladder) Ni Kitu Gani?
Mfuko wa nyongo ni kifuko kidogo sana kama ukubwa wa pera hivi ambacho hutunza nyongo. Kama nilivyoeleza hapo juu,nyongo inayotunzwa kwenye mfuko wa nyongo huzalishwa na ini. Ini huzalisha ml 600 hadi lita moja ya nyongo kwa siku (masaa 24) japo mfuko wa nyongo huweza kutunza ml 40 hadi 60 tu za nyongo kwa mara moja.
Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo-Gallstone
Mawe kwenye mfuko wa nyongo ni miongoni mwa matatizo yenye kuisumbua sana jamii kwa sasa. Ukisikia mawe kwenye mfuko wa nyongo ni vizuri ukafahamu kuwa si mawe halisi bali ni vichembe chembe vigumu hivi vinavyokusanya kwenye kiasi kikubwa hutunzwa kwenye mfuko wa nyongo.
Aina Za Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo
Ziko aina mbili za mawe kwenye mfuko wa nyongo. Aina hizo hutokana na jinsi mawe hayo yanavyosababishwa:
Cholestrol Stones- ni mawe kwenye mfuko wa nyongo yanayosababishwa na kuzidi kwa lehemu (cholestrol) kwenye mfuko wa nyongo. Mawe haya huwa na rangi ya kjani-njano hivi. Ndiyo aina iliyoenea na kuzoeleka sana ya mawe kwenye mfuko wa nyongo.
Pigment Stones- Ni mawe kwenye mfuko wa nyongo yanayotokana na kujikusanya kwa bilirubin (mabaki ya kuvunjwa vunjwa kwa chembe hai nyekundu za damu) kwenye mfuko wa nyongo.
Chanzo Cha Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo
Ziko sababu kuu tatu zinazochangia mawe kujaa kwenye mfuko wa nyongo. Sababu hizo ni kama zifuatazo:
1. Kuongezeka lehemu (cholestrol) kwenye nyongo: kwa kawaida nyongo huzaishwa na ini na kutunzwa ndani ya mfuko wa nyongo. Lakini pia ini huzalisha lehemu japo kuna kiasi fulani cha lehemu huingia mwilini kwa njia ya chakula. Lehemu ikizidi kwenye nyongo husababisha mawe kutokea.
2. Nyongo kujawa na bilirubin nyingi- bilirubin ni mabaki yanayotokana na kuvunjwa vunjwa kwa chembe hai nyekundu za damu (red blood cells) ndani ya ini. Mabaki haya yasipotolewa mwilini hujikusanya na kujazana kwenye mfuko wa nyongo.
3. Nyongo kubakia kwenye mfuko wa nyongo-unapomaliza kula chakula kwa kawaida nyongo yote hutoka na kwenda kusaidia katika umeng'enywaji wa chakula. Kama itatokea mfuko wa nyongo kuachia nyongo kidogo na nyingine kubakia kwa muda mrefu,basi tatizo la mawe ndani ya mfuko wa nyongo hutokea.
Dalili Na Madhara Ya Gallstones
Japo zaidi ya 80% ya wagonjwa wa gallstone hukosa kupata dalili,wachache huweza kukutwa na dalili zafuatayo:
Maumivu makali upande kulia juu ya tumbo
-Kucheua na miungurumo ndani ya tumbo baaada ya kula
-Kutapika mara kwa mara
-Maumivu makali upande wa bega la kulia
-Kutokwa jasho kwa wingi
-Maumivu makali ya mgongo katikati ya mabega
Madhara Ya Gallstone ni kama yafuatayo:
-Kuziba mirija ya nyongo
-Maambukizi kwenye mfuko wa nyongo
-Mrija wa kongosho kuziba
-Manjano
-Kansa ya mfuko wa nyongo
Tiba Ya Mgonjwa Mwenye Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo
Ili tiba ya mgonjwa mwenye gallstone iwe na ufanisi,ni lazima sababu zinazosababisha mawe kutokea. Kuepuka cholestrol nyingi kujikusanya kwenye mfuko wa nyongo na kuondoa bilirubin iliyogandamana kwenye mfuko wa nyongo husaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo hili. Matatizo yote yanayosababisha mawe kutokea husababishwa na matatizo ya ini. Matatizo ya ini kama vile ini kuharibika (liver cirrhosis),ini kuwa na mafuta (fatty liver),homa ya ini (hepatits B,C na D) huweza kusababisha mawe kutokea.
Dawa zetu za kuondoa mawe kwenye mfuko wa nyongo zitakusaidi kuimarisha ini na utendaji kazi wake,kuondoa vyanzo vya mawe kwenye mfuko wa nyongo yaani lehemu,bilirubin na kufungua mirija ya nyongo. Lakini pia utatakiwa kupata virutubishi vya kuimarisha na kujenga ini kwa kuwa hufanya kazi nyingi sana mwilini,zaidi ya kazi mia tano.
Wengi waliotumia dawa hizi kwa ajili ya kuondoa mawe kwenye mfuko wa nyongo,waliahirisha kupata upasuaji,na hawajalalamika tena kuumwa tumbo ama kupata dalili tena ila tu walipokwenda kupima walijikuta mawe hayapo tena na wanaendelea vizuri hadi sasa.
Kama una tatizo hili,ni wakati wako mwafaka kutumia tiba hizi ili kupata ufumbuzi wa tatizo lako.
Jinsi Ya Kudhibiti Mawe Kwenye Mfuko Wa Nyongo
-Kula chakula chenye afya kama vile mboga za majani,matunda na nafaka nzima.
-Kunywa maji mengi kila siku hata kama huna kiu
-Epuka uzito kupita kiasi,jitahidi kuwa na uzito unaoendana na urefu wako.
-Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi kwa wingi
-Epuka kukonda
-Epuka kutumia vidonge vya uzazi wa mpango
-Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa wingi
-Tunza ini lako kuepuka lisidhurike na kuharibika.
Kama una tatizo la mawe kwenye mfuko wako wa nyongo,usisite kuwasiliana nasi upate tiba bora na sahihi kwa ajili ya afya yako. Tuandikie kupitia maishaniafya@gmail.com au tupigie 0673 923 959.