SARATANI YA INI-LIVER CANCER

Saratani ya ini ni aina ya saratani ambayo huanzia kwenye ini. Saratani yoyote inayoanzia nje ya ini na kusambaa hadi kulifikia ini,hiyo... thumbnail 1 summary


Saratani ya ini ni aina ya saratani ambayo huanzia kwenye ini. Saratani yoyote inayoanzia nje ya ini na kusambaa hadi kulifikia ini,hiyo haiitwi kansa ya ini. Mara nyingi kansa ya hepatocellular carcinoma ndiyo kansa iliyozoeleka zaidi kutokea kwenye ini na huanzia kwenye seli za ini zinazoitwa hepatocyte.

Kansa ya ini ni miongoni mwa matatizo hatarishi sana ya kiafya. Kwa mfano nchini Marekani,wanaume elfu 22 na wanawake elfu 9,hugundulika kuwa na kansa ya ini kila mwaka. Katika hao,wanaume elfu 17 na wanawake elfu 8 hupoteza maisha kila mwaka.

Hatari ya mtu kupata saratani ya ini ni kutokana na sababu kuu tatu: kunywa pombe sana,kuwa na hepatitis na kisukari. Saratani ya ini ni miongoni mwa matatizo ambayo dalili zake huonekana katika hatua za badaye za ugonjwa na siyo katika hatua za awali.

Ukiwa na ufonjwa wa saratani ya ini,matibabu yake ni aidha kufanyiwa upasuaji au kubadilishiwa ini. Hebu sasa tuangalie dalili za kansa ya ini:


Dalili Za Kansa Ya Ini



Saratani ya ini katika hatua za baadaye za ugonjwa ni kama zifutazo:

-Njano

-Maumivu upande wa juu wa tumbo

-Kupungua uzito ghafla

-Tumbo kuvimba kwa sababu ya ini kuongezeka ukubwa

-Uchovu

-Kichefuchefu

-Kutapika

-Maumivu ya mgongo

-Miwasho

-Homa

-Kupoteza hamu ya chakula

-Choo cheupe,kama chaki hivi


Hatua Za Kansa Ya Ini



Kujua hatua za kansa ya ini ni muhimu kwa sababu humsaidia daktari kujua ampe mgonjwa tiba gani:

Hatua ya 1: Uvimbe uko kwenye ini pekee na haujaanza kuenea sehemu yoyote

Hatua ya 2: Aidha kuna vimbe mbalimbali kwenye ini,au uvimbe mmoja umefika kwenye mishipa ya damu

Hatua ya 3: Kuna vimbe kubwa nyingi au uvimbe mmoja umefika kwenye mishipa mikuu ya damu. Saratani inaweza pia kuwa imefika kwenye mfuko wa nyongo

Hatua ya 4: Saratani imesambaa kufikia sehemu nyingine za mwili

Inashauriwa tiba kuanza mapema tu baada ya kugundua tatizo. Katika hatua za mwanzo tiba ya kansa na kinga zaidi inaweza kuwa na msaada kwa mgonjwa kuepuka madhara zaidi.


Chanzo Cha Kansa Ya Ini



Chanzo cha kansa ya ini bado hakijafahamika. Ila maambukizi ya hepatitia B na C ni kichocheo kikubwa cha kansa ya ini. Kulingana na jamii ya kansa ya Marekani,hepatitis C ni chanzo kikubwa cha kansa ya ini na hepatitis B.


Sababu Hatarishi Za Ugonjwa Wa Kansa Ya Ini



Unaweza kuwa katika hatari ya kupata kansa ya ini kama unaweza kupatwa na matatizo yafutayo:


Maambukizi sugu ya Hepetitis B na C-virusi wanaosababisha hepatitis b na c huongeza hatari yako kupata saratani ya ini

Cirrhosis-ni hatua endelevu isiyotibika inayosababisha tishu zenye makovu kutengenezwa kwenye ini lako,na hii huongeza hatari ya kupatasaratani ya ini

Magonjwa ya kurithi-magonjw aya kurithi kama hemochromatosis na wilson's disease huongeza hatari ya kupata kansa ya ini

Kisukari-watu wenye kisukari,wana hatari kubw aya kupata kansa ya ini kuliko wasio na ugonjwa wa kisukari.

Nonalcoholic fatty liver disease-kuongezeka kwa mafuta kwenye ini huongeza hatari na uwezekano wa kupata ugonjwa wa kansa ya ini

Sumu ya aflatoxin-ni sumu inayopatikana kwenye mazao yasiyohifadhiwa vyema. Kwa mfano mahindi na karanga huweza kuvamiwa na sumu hii. Nchi Marekani sheria ngumu imewekwa kuhakikisha sumu ya aflatoxin haitokei

Pombe-kunywa pombe kwa wingi kwa muda mrefu hupelekea matatizo yasiyo na tiba ya ini na kuhatarisha kupata kansa ya ini

Kinga duni-watu wenye kinga dhaifu,mfano wenye VVU/UKIMWI wako katika hatari kubwa ya kupata saratani ya ini

Unene kupita kiasi-uzito au mwili usiokuwa mnene kupita kiasi,huepusha magonjw amengi ikiwemo kansa ya ini

Kuvuta sigara-huongeza hatari hasa kwa wagonjwa wenye hepatitis B na C

Jinsia-wanaume wengi wako katika hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya ini kuliko wanawake

Sumu ya  Arsenic-sumu hii huweza kupatikana kwenye maji kwa asili. Kunywa maji safi na salama  jambo hupunguza hatari ya kupata kansa ya ini.


Jinsi Ya Kuepuka Kansa Ya Ini



Fanya mambo yafuatayo kuepuka kupata saratani ya in:

-Punguza unywaji pombe-kama hujaweza kuacha kunywa pombe punguza kunywa na ukiweza acha kabisa

-Dumisha uzito unaotakiwa-fanya kila linalowezekana kudumisha kiwango cha uzito unaotakiwa,ili kuwa katika hali ya kuepuka ini lako kuharibika

-Tumia kemikali kwa tahadhali-kuwa mwangalifu wakati unatumia kemikali yoyote kuepuka matatizo ya ini yanayoweza kupelekea cirrhosis

-Pata chanjo ya hepatitis b

Jihadhari na hepatitis C kwa:

-Kuepuka ngono isiyo salama

-Kuchukua tahadhari katika kutumia vitu vyenye ncha kali


Hii ndiyo kansa ya ini. Ni afadhali ufanye kila kinachowezekana kuepuka kupata kansa ya ini,kuliko kujiachia ukategemea kupata tiba baada ya kupata saratani ya ini. Unaweza kufanya kila linalowezekana kulinda afya ya ini lako na kuepukana na hatari ya saratani ya ini.


Kuanza tiba ya ini,bofya hapa:

Wasiliana nasi kupitia afyagreen@gmail.com au tupigie +255 673 923 959.