Kampuni ya Green World ni kampuni ya kimataifa yenye makao makuu Michigan Marekani. Kampuni hii ilianzishwa rasmi mwaka 1994 huko Michigan Marekani. Ilianzishwa na Dkt. Deming Li mzaliwa wa China na mwenye uraia wa marekani,alikuwa na nia njema kabisa ya kuwasaidia watu pote duniani kutumia mimea ili kuimarisha afya na kuepukana na magonjwa na matatizo mengi yaliyo sugu.
Ili kufanikisha adhima hiyo aliamua kufanya utafiti wa kina kubaini chanzo na tabia za magonjwa mengi ili kutafuta suluhisho lake. Alianzisha kituo cha utafiti huko Michigan Marekani mapema mwaka 1994. Kituo hiki kilifanyia utafiti ufanisi na wa tiba za kiasili za kichina zilizotumika zamani sana na kuwa na ufanisi wa watu wengi. Lakini kupitia kituo hiki pia,utafiti maalumu na mahususi juu ya magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya huko Michigan Marekani.
Tafiti hizi ziliendana sambamba na kusoma kwa umakini elimu ya madawa ya asili ya kichina,yaliyotokana na mimea,mizizi au madini yaliyotumiwa na wazee wa miaka mingi wakiwemo watawala ili kutibu afya zao.
Baada ya utafiti wa muda mrefu na wenye mafanikio,ndipo alipoanzisha mashamba makubwa ya kuzalisha mimea ya kutosha huko nchini kwao China. Mwaka 1997 kiwanda kikubwa cha kuzalisha virutubisho na bidhaa tiba kwa ajili ya matumizi ya binadamu kilijengwa mjini Tianjin nchini China,na bidhaa hizi zikaanza kutumika tokea hapo.
Baada ya hapo kampuni ya Green world ikaaamua kusambaza bidhaa zake kwa njia ya biashara ya mtandao (Network Marketing),ili kuzifikia nchi nyingi kwa haraka wakianza na nchi za Ulaya na Asia.Kwa sababu uhitaji umezidi kuongezeka kila kunapokucha kampuni imejenga kiwanga kingine kwa ajili ya uzalishaji katika jiji la Nanjing hapo hapo nchini china.
Kuingia Kwa Green World Afrika
Mwaka 2007 ndipo kwa mara ya kwanza kampuni ya Green world ilipotambulishwa na kusajiliwa nchini Afrika kusini,ikiwa ni nchi ya kwanza kabisa. Mara hii ililetwa na Mr. David Zhang ambaye ni Makamu mwenyekiti wa Kampuni hii duniani. Hadi sasa kuna nchi zaidi ya 23 ambazo tayari kuna matawi ya kampuni ya Green world Afrika,ikiwemo na Tanzania.
Kuingia Kwa Green World Tanzania
Hapa nchini kwetu Tanzania kampuni ya Green world imesajiriwa rasmi 9 septemba 2008. Tokea wakati huo watanzania wamekuwa wakinufaika kiuchumi na kiafya kupitia bidhaa na mfumo wa biashara wa kampuni ya Green world. Hadi leo,kuna nchi zaidi ya 70 zenye wanachama na watumiaji wa bidhaa za Green world. Kwa Afrika ni zaidi ya nchi 23 ikiwemo na Tanzania.
More products
Kwa maelezo ya kina na msaada wa karibu,wasiliana nasi kupitia simu 0673 92 39 59.