Kuna aina nyingi za mbolea ambazo mkulima unaweza kuzitumia katika bustani au shamba lako ili kukusaidia kupata mavuno mengi na bora zaidi. Katika mada yetu ya leo tutaizungumzia aina mpya ya mbolea inayotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Green World. Tofauti ya aina hii ya mbolea na nyingine nyingi ambazo hutumika kwa kuzifukia ardhini, aina hii mpya hutumika kwa kunyunyizia kwenye majani ya mmea. Kabla ya kuanza kuijadili aina hii mpya ya mbolea, hebu tujikumbushe kidogo historia ya matumizi ya mbolea kwenye nchi zetu za Afrika.
Kabla ya ujio wa wazungu, waafrika tulikwishajua umuhimu wa kutumia mbolea na mbolea za samadi ndizo zilizotumika. Baadaye elimu ilitufunza namna ya kutengeneza mbolea kwa kufukia nyasi, kinyesi cha mifugo na vitu vingine kwenye mashimo yaliyochimbwa na kuvifukua baada ya muda fulani – biwi.
Baadaye, baada ya kupata uhuru, tuliletewa aina nyingine za mbolea ambazo zilitengenezwa viwandani. Mbolea hizi ni za sulphates, phosphates na nitrates. Nchini Tanzania tunazijua mbolea zilizotengenezwa mjini Tanga. Kuna Single Super Phospahte (SSP) au calcium dihydrogen phospahte (Ca(H2PO4)2) na Triple Super Phosphate (TSP)ambazo hutengenezwa kutokana na mawe kutoka eneo la Minjingu-Arusha. Aina nyingine iliyozoeleka ambayo pia hutengenezwa mjini Tanga, ni Ammonium Sulphate (NH4)2SO4). Aina nyingine za mbolea, ambazo zimekuwa zikiagizwa kutoka nchi za nje, ni Ammonium Nitrate na Calcium Ammonium Nitrate.

Mbolea Ya Aina Mpya Ya Kampuni Ya Green World
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameonyesha kuwa mmea unaweza pia kupata chakula chake kupitia majani na ukawa kamilifu kabisa. Matokeo ya ugunduzi huo umetuletea aina mpya za mbolea. Mojawapo ya mbolea hizo mpya ni mbolea ya maji inayoitwaNutriplant Organic Plus Fertilizer (NOPF) inayotengenezwa na kampuni ya Green World. Mbolea hii inatunzwa ndani ya plastiki ndogo yenye ujazo wa lita moja na hutumika kwa kunyunyizia kwenye majani ya mmea. Utengenezaji wa mbolea hii umezingatia mahitaji yote ya mmea ikiwa ni pamoja na virutubisho vyote vinavyohitajika kwa wingi na mmea (macronutrients) ambavyo ni Nitrogen, Phosphorus, Potassium, Calcium, magnesium na Sulphur, na vyote ambavyo vinayohitajika kwa kiwango kidogo (micronutrients), vikiwa ni Ferrous, Zinc, Copper, Boron, Manganese, Silicon, Molybdenum, Sodium, Cobalt na Chlorine.
Kwa vile amino acids ni muhimu katika ukuaji wa mmea, mbolea hii imejumuisha aina zote 18 za amino acids. Pamoja na ukuaji wa mmea, amino acids huupa mmea sifa nyingine nyingi sana, mfano; uwezo wa kupambana na magonjwa na wadudu, ukuaji wa haraka n.k.

Tofauti Ya Mbolea Ya Green World Na Mbolea Nyingine
Mbolea za nitrates, sulphates na phospahtes hutengenezwa viwandani, kwa hiyo ni mbolea za kemikali. Mbolea hizi kiutaalamu huitwa Inorganic Fertilizers. Aina hii mpya ya mbolea inayotengenezwa na Green World, haitokani na kemikali bali na wanyama na mimea. Organic maana yake kitu kilichotokana na viumbe hai – kitu kinachotokana na mimea au wanyama. Kuna tofauti kubwa kati ya kutumia mbolea za kemikali na mbolea za organiki. Tofauti kuu ni:
1. Mbolea ya Green World ina virutubisho vyote, vile vinavyohitajikakwa wingi na mmea, macronutrients, na vile vinavyohitajika kwa kiwango kidogo, micronutrients. Mbolea za kemikali hutengenezwa zikiwa na macronutrients tu.
2. Mbolea za Green World ni rafiki wa mazingira. Wakati ukiendelea kuitumia mbolea hii, mazingira yako hayaharibiki tofauti na matumizi ya mbolea za kemikali ambazo huharibu mazingira.
3. Mbolea za Green World zinatumika kwa muda mrefu na kuendela kukuletea mazao bora wakati mbolea zingine hutumika kwa muda mfupi kabla ya kuanza kudorora kwa uzalishaji.
4. Mbolea za Green World huongeza ubora wa mazao, kama ukubwa, rangi, ujazo na ladha. Mbolea nyingine za kemikali hupunguza ubora wa mazao.
5. Mbolea za Green World huboresha udongo wa shamba lako. Unaweza kuitumia kutibu ardhi iliyochoka. Mbolea hii hurudishia pH ya udongo hadi kiwango kinachohitajika na mimea cha kati ya 6-8. Mbolea za kemikali huzidisha pH ya udongo, hatimaye kuufanya udongo wa shamba lako kuwa haufai kwa mimea.
Faida Za Kutumia Mbolea Ya Green World
Uwingi Wa Amino Acids: Matumizi ya mbolea ya Green World yana faida nyingi kwenye mimea yako. Mbolea hii huupa mmea wako amino acids zote zinazohitajika na mmea ili kuufanya ukue kwa haraka, ujikinge na wadudu, usipate maradhi kiurahisi na mengineyomengi.
Matumizi Kwa Eneo Kubwa: Mbolea hii imesheheni virutubisho vingi katika ujazo mdogo na kukuwezesha kuongeza maji mengi ili itumike kwenye eneo kubwa zaidi. Kichupa hiki cha lita 1 kinatakiwa kichanganywe na maji yenye ujazo wa lita 1000 kiasi ambacho kinaweza kunyunyiziwa kwenye shamba la ukubwa wa hekta 6.7 au eka 16.5. Kama shamba lako ni dogo unaweza kujaza mbolea kwenye kifuniko cha chupa hiyo ambacho kina ujazo wa ml 50 na ukachanganya na maji lita 50. Kwa kipandekidogo cha bustani unaweza kuchangaya cc 5-10 kwenye lita 20 za maji na kunyunyizia kwenye kijieneo chako.
Salama Kwa Binadamu Na Mifugo: Mbolea ni salama kwa afya ya binadamu na mifugo. Unaweza kuchuma mboga au matunda yaliyonyunyiziwa mbolea na kuyala au mnyama akala majani yaliyonyunyiziwa mbolea bila kupata madhara.
Matokeo Ya Haraka: Mabadiliko kwenye mmea ulionyunyiziwa mbolea huoneka baada ya siku chache – siku kama 7 baada ya matumizi ya mbolea hii.

Namna Ya Kutumia Mbolea Ya Green World
Njia nyingi sana zinaweza kutumika katika kunyunyiza mbolea. Kwenye mashamba makubwa ya mboga na mimea mingine mifupi, vifaa vya kunyunyiza mbolea kama mvua kwenye eneo kubwa vinaweza kutumika. Shamba la miti ya matunda linaweza kunyunyiziwa kupitia mizizi. Drip irrigation pia inaweza kutumika kulingana na mazingira. Mtu mwenye kijieneo kidogo anaweza kutumia kifaa cha kubeba mgongoni na akanyunyiza mimea yake.
Mbolea hii inatakiwa kuinyunyizia kwenye mimea mapema asubuhi kabla ya saa 3 au jioni baada ya saa 10. Haifai kutumika wakati wa jua kali.
Endapo baada ya kuinyunyizia mbolea mvua ikanyesha, inatakiwa kunyunyiza tena mbolea baada ya saa 24 toka mvua ilipokatika.
Mimea midogo ya mbogamboga inatakiwa kunyunyiziwa kila baada ya siku 7 hadi 10 na mimea mikubwa ya matunda kunyunyiziwa kila baada ya siku 20.
Ili mbegu ziote kwa haraka, unaweza kuloweka mbegu zako kwenye mbolea kwa saa 8 kabla ya kuzipanda.
Kutambuliwa Kwa Mbolea Hii
Baadhi ya serikali za nchi zilizopata mbolea hii siku nyingi kidogo, zimefanya utafiti wa kina kuona ubora wa mbolea hii kabla ya kuipasisha. Kwa mfano, serikali ya Nigeria kupitia wizara yake husika (Federal Ministry of Agriculture and Rural Development of Nigeria) imeipasisha mbolea hii tarehe 2 Machi 2016 baada ya wataalamu wao kuichunguza mbolea hii kwa miezi miwili katika maabara zao na kuona inafaa kabisa kwa matumizi nchini mwao. Kusoma zaidi ingia hapa:
Nchini Tanzania, samples zipo mwikononi mwa vyombo (TFRA) husika na mategemeo ni kuwa siku za usoni itapasishwa rasmi.
Upatikanaji wa Mbolea Ya Green World
Kama umependa kutumia mbolea ya Green World kwa kilimo chako, wasiliana nasi kwa kutumia namba 0673 923 959 Unaweza pia kufanya biashara ya mbolea hii kama utajiunga na fursa ya biashara ya kampuni yetu ya Green world.